LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATOTO MKOANI MWANZA WAIOMBA SERIKALI KUENDELEZA VIPAJI VYAO. WASEMA ITASAIDIA KUPUNGUZA ONGEZEKO LA WATOTO MITAANI.

Watoto kutoka Baraza la Watoto Mkoa wa Mwanza wakiwa katika Picha ya Pamoja na Davis Justine ambae ni Afisa Maendeleo ya Jamii, idara ya Watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi kutoka Jiji la Mwanza (Mwenye Miwani).

Baraza la Watoto Mkoa wa Mwanza limeiomba Serikali kuanzisha na kusimamia vituo mbalimbali vya Michezo hapa nchini, kwa lengo la kukuza na kuendeleza Vipaumbele vyao ambavyo ni
Vipaji vya aina mbalimbali.


Watoto hao wameyasema hayo jana wakati wakizungumza na Davis Justine ambae ni Afisa Maendeleo ya Jamii, idara ya Watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi kutoka Jiji la Mwanza, kupitia mradi wa Jiji langu Sauti yangu ambao unaendeshwa na Mtandao wa Watoto na Vijana Mkoani Mwanza (MYCN).


Wamebainisha kwamba wao kipaumbele chao kikubwa ni Vipaji, hivyo kama kipaumbele hicho kitaendelezwa itakuwa rahisi watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi kuondokana na tatizo la wao kuishi Mitaani kwa kuwa kama kutakuwa na Vituo vya kuendeleza vipaji vyao wataweza kujinasua kutoka Mitaani na kuvitumia vipaji vyao kujiendeleza kimaisha.


Watoto hao wamependekeza kuwa Serikali kwa kuanza, inaweza kuteua baadhi ya Shule za Msingi ama Sekondari hapa nchini kwa ajili ya kuziboresha na kuwa Vituo vya Kukuza na Kuendeleza Vipaji vya Watoto.

Kuhusiana na Suala la Ongezeko la idadi ya Watoto wanaoishi Mitaani, Watoto hao wamebainisha kuwa suala hilo limekuwa likisababishwa na sababu mbalimbali huku nyingi zikiwa ni za kifamilia ambazo ni pamoja na ugumu wa Maisha katika familia, watoto Kutendewa Ukatili wa aina mbalimbali na wazazi ama walezi wao ama watoto kufiwa na Wazazi.
Davis Justine ambae ni Afisa Maendeleo ya Jamii, idara ya Watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi kutoka Jiji la Mwanza

Akijibu ombi la Watoto hao, Davis Justine ambae ni Afisa Maendeleo ya Jamii, idara ya Watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi kutoka Jiji la Mwanza amesema kuwa ombi la watoto hao ni la msingi hivyo atalifikisha katika ngazi husika kwa ajili ya kushughulikiwa, huku akibainisha kuwa tangu awali suala la kutambua vipaji vya watoto limekuwa likifanyika japo limekuwa likisimamiwa na taasisi za watu binafsi.

Davis Justine ambae ni Afisa Maendeleo ya Jamii, idara ya Watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi kutoka Jiji la Mwanza (Kulia) na Kushoto ni Brightius Titus ambae ni Katibu Mkuu wa MYCN

Lengo la Watoto hao kukutana na Viongozi kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza kupitia Mradi wa Jiji langu Sauti yangu unaosimamiwa na Mtandao wa Watoto na Vijana Mkoani mwanza, ni kwa ajili ya kukuza na kuchochea Maendeleo ya Watoto na kuwaondoa katika changamoto mbalimbali zinazowakabili ambazo ni pamoja na watoto kukimbilia Mitaani kutokana na kukosa malezi bora na hivyo kupoteza dira Kimaisha

Watoto kutoka Baraza la Watoto Mkoa wa Mwanza.
Watoto kutoka Baraza la Watoto Mkoa wa Mwanza.
Watoto kutoka Baraza la Watoto Mkoa wa Mwanza.
Wanahabari kutoka City FM (Kushoto) na RFA (Kulia).
Watumishi wa MYCN.
Watumishi wa MYCN.
Taswira ya Kikao kilichofanyika katika Ofisi za MYCN zilizopo Ghana Ilemela Mkoani Mwanza Ilivyokuwa.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.