LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAINE MTUKA MSANII KUTOKA SOUND LAB STUDIO AACHIA NGOMA MPYA.

Msanii wa Kizazi Kipya Maine Mtuka.
Maine Mtuka ni Msanii wa Kizazi Kipya kutoka Misungwi Mkoani Mwanza ameachia Ngoma yake ya Kwanza ambayo
amefanyia katika Studio ya Sound Lab iliyoko Usagara-Misungwi Mkoani Mwanza ikiwa ni Mkono wa Producer Dashi Touch.

Ikiwa ni ngoma yake ya Kwanza, lakini kwa namna ambavyo Maine Mtuka amesimama katika ngoma hiyo huwezi jua kama ni Msanii mpya kwenye mziki huu wa Kizazi Kipya jambo ambalo linadhihilisha kauli aliyoitoa wakati akizungumza na Radio Metro kwamba, hajakurupuka kuingia kwenye game bali ilimchukua kipindi kirefu akijifua.

"Unajua wasanii wengi wanaingia katika mziki kila kukicha, lakini ukija kuangalia ambao huwa wanafanikiwa huwa ni wachache sana kulinaganisha na idadi ya wanaoingia. Mimi nilitumia muda mwingi kujiandaa kwa ajili ya kuingia kwenye mziki na hatua hii niliyofikia nina uwezo mkubwa sana na naweza kufanya kazi na ikaeleweka kwa wasikilizaji" Alieza Mtuka.

Ngoma ambayo ameiachia Maine Mtuka inafahamika kama ZA WAPI ambapo katika hiyo ngoma amesimama peke yake ikiwa ni ujio wake wa kwanza kabisa, hakika ni ngoma nzuri. ISIKILIZE HAPA CHINI Kisha mshauri kupitia namba 0768 16 96 58 au Mshauri wake 0769 10 39 52.


Msanii wa Kizazi Kipya Maine Mtuka.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.