LIVE STREAM ADS

Header Ads

ALAZWA HOSPITALINI BAADA YA KUMEZA SIMU YENYE MSG ALIZOTUMIWA NA MCHEPUKO AKIWA NA MPENZI WAKE.Binti Mmoja mwenye umri wa miaka 19 ambae kutokana na sababu mbambali jina lake limehifadhiwa, amelazwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kumeza simu yake ya mkononi.


Kisa cha binti huyo ambae ni raia wa Brazil kumeza simu hiyo kimetokana na kutumiwa msg za kimapenzi na Mchepuko wake huku akiwa na Mpenzi wake jambo ambalo lilimuweka katika wakati mgumu baada ya mchumba wake huyo kutaka kuichukua simu hiyo kwa minajiri ya kusoma msg alizokuwa ametumiwa.

Kabla ya Binti huyo kumeza simu hiyo, kulitokea mvutano mkali baina ya wawili hao ambao ni mtu na mchumba wake, kabla ya binti huyo kuchukua maamuzi hayo magumu ya kubugia simu yake hiyo iliyokuwa na msg za kimahaba kutoka kwa mchepuko wake.

Madaktari wanaomtibu binti huyo wanasema kuwa bado hali yake haijatengamaa na wanaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa wanaokoa uhai wake ambapo taarifa zaidi zinaeleza kuwa huenda binti huyo akalazimika kufanyiwa upasuaji ili kufanikisha zoezi la kuitoa simu aliyoimeza.

Ama hakika Michepuko ni Noma Sana. Baki Njia Kuu ili kuepukana na dhahma kama hii iliyomkumba binti huyu, ukiachilia mbali dhahma nyinginezo kama vile Magonjwa ya zinaa kama vile maambukizi ya virusi vya Ukimwi ama Vipigo kutoka kwa wenye Mali.
 Na: George Binagi @ 99.4 Metro FM & Mtanzania Media-Kwa Hisani ya Mtandao.

No comments:

Powered by Blogger.