“Hata kama utazaliwa na kipaji, jua lazima ufanye mazoezi.
Mfano mimi ni kweli nimezaliwa na kipaji lakini
nilikuwa sijui jinsi ya
kukitumia. Nilikua naimba utadhani najiimbia mimi mwenyewe, kumbe napaswa
kuimba kwa ajili ya wanaonisikiliza. Mimi hilo sikulijua hapo awali hadi pale
nilipofundishwa jinsi ya kukitumia kipaji change”.
Hayo yalikuwa ni maneno kutoka kwa mwanadada Maryan aka Super Queen alipokuwa
akizungumza na Mtanzania Media Blog juu ya ujio wa kazi yake mpya ambayo ni
kazi yake ya pili ambayo ameiachia rasmi hii leo. Mdada huyu anawakilisha Rock
City Mwanza-Mwanza.
Ngoma yake ya kwanza ambayo pia ilimpa shavu la kutengeneza
ngoma ya pili ilikuwa inafahamika kwa jina la “ISHI NA MIMI” na ni ngoma ambayo ukiisikiliza utajua kweli bi-dada
ana kipaji cha hali ya juu. Kama ni kuimba, anaimba kweli na habanii sauti.
Yote tisa, Kumi ni katika hii ngoma mpya aliyoiachia hii leo
Maryan ambayo inakwenda kwa jina la “TUSONGE”
ikiwa ni mkono wa Double K Classic kutoka Rock Town Records Jijini Mwanza.
Mzigo umesimama kiukweli, na Mtoto anajua kuimba. Mcheck kupitia namba 0657 36 96 66 kwa kazi zaidi.
|
No comments: