LIVE STREAM ADS

Header Ads

NEW HIT SONG: CHONGOROA BY NYASA BOY FT. D-MARADHA & MC-DARADA.

MKALI KUTOKA ROCK CITY-NYASA BOY.


Ama hakika ushindani wa Soko la Mziki kwa hapa nchini unazidi kuwafanya wasanii kuumizwa vichwa vyao ili wanapoingia studio kurekodi ngoma, basi waweze kutoka na ngoma zenye ujazo unaoweza kuwabamba mashabiki zao.


Ushindani huo huo ndio pia uliomfanya
Msanii Nyasa Boy kutoka Jijini Mwanza kuumiza kichwa na hatimae kuja na ngoma kali ambayo kwa hivi sasa ni gumzo katika Jiji la Mwanza na viunga vyake sanjari na Radio mbalimbali hapa nchini.


Jamaa huyu amejikuta anapata mapokezi ya hali ya juu baada ya kuachia ngoma yake inayofahamika kama “CHONGOROA”. Humo ndani amemshirikia MC-Darada pamoja na D-Maradha wote kutoka Rock City na Mzigo huo umesukwa Mnyambudu Touch.


Kwa ngoma zilizoachia hivi karibuni hususani Jijini Mwanza, Ngoma hii imeongoza kwa kuwa ngoma inayoombwa zaidi na wasikilizaji katika vituo mbalimbali vya Radio Jijini Mwanza na inakoelekea ni kubaya maana itapoteza mbaya.


Mshikaji anasema ana ndoto za kuendelea kufanya kazi nzuri na bora na kwa hivi sasa yuko katika harakati za kutafuta warimbwende wa kuweza kung’arisha kichupa cha ngoma hiyo, hivyo kama wewe unajua ni mrimbwende na unaweza kutisha katika ngoma hiyo, basi mcheki mshikaji kwa namba 0759 21 19 77 ili mpige nae Kichupa.  
ISIKILIZE NA KUIDOWNLOAD NGOMA HIYO HAPA CHINI.

MKALI KUTOKA ROCK CITY-NYASA BOY AKIWA KATIKA STUDIO ZA 99.4 METRO FM JIJINI MWANZA.
 Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.