LIVE STREAM ADS

Header Ads

BARABARA ILIYOSHINDIKANA MIAKA MINGI JIJINI MWANZA, YAANZA KUFANYIWA UKARABATI. WATUMIAJI WAKE WANENA.

"HII BARABARA SIJUI INA NINI. LAKINI NADHANI HUU  NI MRADI WA BAADHI YA WATU, HAIWEZEKANI HII BARABARA KILA IKIFANYIWA UKARABATI HAIMALIZI HATA MWAKA INAKUWA MASHIMO KILA SEHEMU. HAPA KUNA WATU WAPIGA HELA." WALIEZA.

Madereva wa daladala na watumiaji mbalimbali wa Barabara ya Pamba iliyopo Jijini Mwanza, wameitaka Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuhakikisha kwamba Mkandarasi anaefanya ukarabati barabara hiyo kuhakikisha kuwa ukarabati wake unakuwa wa kudumu.

Wametoa tamko hilo mapema hii leo wakati wakizungumza na Mtanzania Media juu ya ukarabati wa barabara hiyo, ambayo wamesema kwamba kwa miaka mingi imekuwa sugu kutokana na kufanyiwa ukarabati wa mara kwa mara bila mafanikio yoyote.

Wameeleza kwamba barabara hiyo kwa miaka mingi imekuwa kama mradi wa baadhi ya Watu Jijini Mwanza, kwa kuwa marekebisho ambayo yamekuwa yakifanyika yamekuwa hayadumu, hali ambayo imekuwa ikisababisha kero kubwa kwa watumiaji wake hususani madereva wa magari kutokana na mashimo ambayo yamekuwa yakitokea katika kipindi kifupi baada ya ukarabati kufanyika.

Mtanzania Media imeshuhudia ukarabati mkubwa ukifanyika katika barabara hiyo na Kampuni ya Jasco, ambapo ukarabati wake umeanza katika hatua ya mwanzo kabisa baada ya mkandarasi huyo kuitifua upya na kuanza kuijanza moram upya kabla ya kuweka lami.
Haijabainika Ukarabati huu utadumu kwa muda gani sanjari na Kiasi cha fedha kilichotengwa kutumika ambapo Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Halifa Hida akizungumza na Mtanzania Media kwa njia ya Simu mapema leo, ameahidi kuwasiliana na Mhandisi anaesimamia ukarabati huo ili kupata majibu sahihi juu ya maswali hayo kabla ya kuyaweka bayana.
Kipande kinachofanyiwa Ukarabati ni kile kilichopo kuanzia eneo la Sahara Conner hadi eneo la Jengo la Kishimba sanjari na kipande kilichopo katika kona inayotoka Sahara kwenda Buhongwa. Tusubiri tuone matokeo ya Ukarabati huu.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.