Hili ni Jengo la Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoani Mwanza (MWAUASA). Jengo hili lipo eneo la Isamilo Jijini Mwanza. Sina uhakika ni la Ghorofa ngapi maana ujenzi bado unaendelea, lakini mpaka sasa
limefikia zaidi ya ghorofa tatu na inaonekana bado kuna nafasi ya ujenzi kwenda juu zaidi. Watalaamu mnaweza kutusaidia, JE NYUFA HIZI ZINAZOZIBWA HIVI, HAZIWEZI KULETA ATHARI HAPO BAADAE?JAPO BAADHI WANASEMA NYUFA HIZO HAZINA MADHARA YOYOTE MAANA NDANI YAKE KUNA NDONO, JAPOKUWA NDONDO HIZO INAONEKANA ZILICHAKACHULIWA HIVYO ZIMESHINDWA KUHIMILI NGUZO HIZO NDIYO MAANA NYUFA ZINATOKEA.
Ni maalumu kwa ajili ya kuwa Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo. Cha kushangaza ni kwamba, licha ya ujenzi wa jengo hilo kuwa wa kusua sua, lakini kiwango chake cha ujenzi kinatia huruma. Shuhudia VIRAKA katika jengo hilo hata kabla ya ujenzi kukamilika.Kwa mfumo huu, naiona hatari ya majengo kuzidi kudondoka hapa nchini hata kabla ya kukamilika ujenzi wake. |
No comments: