LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHUGHULI ZA KILOMO KANDO KANDO YA ZIWA VICTORIA ZAKWAMISHA MAPAMBANO DHIDI YA GUGU MAJI.

Fredirick Mhina Mgube (Kushoto) ambae ni Afisa Mazingira na Maliasili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, anaeshughulikia Mradi wa Mazingira wa LIVEMP II ambao unapambana na Gugu Maji katika inchi zote tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kulia ni Martini Katua ambae ni Mratibu wa Shughuli za udhibiti wa gugu maji katika Mradi wa Hifadhi ya Mazingira ya Ziwa Victoria nchini Tanzania na Katikati ni Jane Masso ambae ni Mwenyekiti wa Mradi wa Udhibiti gugu maji Kirumba Kati Mkoani Mwanza.
Shughuli za Kilimo Kando Kando ya Ziwa Victoria, zimetajwa kuwa Changamoto kubwa inayokwamisha mapambano dhini ya Gugu Maji katika Ukanda wa Ziwa Victoria hali ambayo imetajwa kuhatarisha uhai wa Ziwa hilo sanjari na viumbe vilivyomo.

Hayo yalibainishwa jana na Fredirick Mhina ambae ni Afisa Mazingira na Maliasili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, anaeshughulikia Mradi wa Mazingira wa LIVEMP II ambao unapambana na Gugu Maji katika inchi zote tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhina aliyasema hayo Mkoani Mwanza wakati akijionea shughuli za uondoaji wa Gugu Maji kando Kando ya Ziwa Victoria, zinazofanywa na Mradi wa Udhibiti gugu maji kutoka Kata ya Kirumba, zinazoendelea kando kando mwa ziwa hilo eneo la Nera Jijini Mwanza.

Ili kufanikisha mapambano dhini ya gugu maji katika Ziwa Victoria na Ukanda wote wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhina aliwataka wananchi kushirikiana na viongozi wa Serikali na taasisi mbalimbali katika kulilinda ziwa Victoria ikiwa ni pamoja na kusitisha shughuli zote za kilimo kando kando ya Ziwa Victoria.
Kwa Upande wake Martini Katua ambae ni Mratibu wa Shughuli za udhibiti wa gugu maji katika Mradi wa Hifadhi ya Mazingira ya Ziwa Victoria nchini Tanzania, alibainisha kuwa gugu maji limekuwa ni tatizo kwa kipindi kirefu lakini juhudi za kuhakikisha kwamba linatomozwa zimeanza kufanikiwa.

Alibainisha kuwa juhudi za kupambana na gugu maji zimeanza kuonyesha mafanikio ambapo tafiti zinaonyesha kwamba kwa mwaka 2010 kulikuwa na takribani hekta 520 za gugu maji ndani ya Ziwa Victoria, ikilinganishwa na tafiti zilizofanyika mwezi wa tano mwaka huu ambazo zilibaini kuwepo kwa hekta 164 za gugu maji kwa hivi sasa ambapo bado juhudi zinazidi kufanyika ili kuhakikisha kuwa gugu maji hizo zinaondolewa ndani ya Ziwa Victoria.
Juhudi za kupambana na gugu maji ndani ya Ziwa Victoria zinazidi kupamba moto kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali, ambapo kwa Mkoa wa Mwanza Jane Masso ambae ni Mwenyekiti wa Mradi wa Udhibiti gugu maji kutoka Kirumba Kati pamoja na Costantin John Manyerere ambae ni Mwenyekiti wa BMU (Beach Management Unit) Kata ya Kirumba, kwa pamoja wanasema kuwa wataendelea kushirikiana na mradi wa udhibiti wa gugu maji ndani ya Ziwa Victoria unaosimamiwa na LIVEMP II ili kuhakikisha kuwa gugu maji linatokomezwa kabisa.
Juhudi hizo pia zinaungwa mkono na Diwani wa Kata ya Kirumba (Chadema) Kahungu Dani ambae amekuwa akihamasisha wananchi kujiepusha na shughuli za kilimo kando kando ya ziwa Victoria ambapo kwa upande mwingine ameomba taasisi mbalimbali za binafsi na serikali kujitokeza katika kuwawezesha wananchi wanaoshughulikia uondoaji wa gugu maji ndani ya Ziwa Victoria.
Miongoni mwa sababu kubwa zinazopelekea mapambano dhidi ya gugu maji ni pamoja na athari zake ambazo ni pamoja na uhai wa viumbe vya majini wakiwemo samaki sanjari na kupungua kwa kina cha maji hali ambayo ambayo inaweza kuhatarisha kutoweka kwa Ziwa.
Shughuli ya Kuondoa gugu maji ikiendelea katika eneo la Nera Jijini Mwanza.
Hili ni gugu maji lililopo kando kando mwa ziwa Victoaria katika eneo la Nera Jijini Mwanza likiwa limetawaliwa na gugu maji ambapo juhudi za kuliondoa zinaendeleo kwa ushirikiano wa Mradi wa kudhibiti gugu maji Kirumba Kati, BMU Kata ya Kirumba wadau wengine akiwemo Diwani wa Kirumba pamoja  na LIVEMP II.
Kilimo cha Mboga Mboga nayo kando kando ya Ziwa Victoria ni changamoto nyingine ya kukabiliana na Magugu Maji katika Ukanda wa Ziwa hilo. Hapa ni eneo la Nera Jijini Mwanza ambapo Kilimo pia imekuwa ni changamoto inayokwamisha mapapambano dhidi ya Gugu Maji katika Ziwa Victoria. 

"Ili kutokomeza hali hii, sheria zinazodhibiti shughuli mbalimbali kando kando ya vyanzo vya maji inapaswa kuzingatiwa" Akishauri Fredirick Mhina ambae ni Afisa Mazingira na Maliasili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, anaeshughulikia Mradi wa Mazingira wa LIVEMP II ambao unapambana na Gugu Maji katika inchi zote tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.