LIVE STREAM ADS

Header Ads

MGOMO WA WAFANYABIASHARA JIJINI MWANZA KUMUONDOA MKURUGENZI WA JIJI MADARAKANI.

Viongozi wa Jumuia ya Wafanyabiashara Mkoani Mwanza, wakizungumza na Waandishi wa Habari mapema asubuhi ya leo, muda mfupi tu baada ya kutoa taarifa kwa wafanyabiashara Jijini Mwanza ili kufungua maduka yao, Na hapa walikuwa katika Stand ya Tanganyika ambapo walikuwa wakitoa taarifa pia juu ya kilichojili jana katika kikao baina yao na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.
Mgomo wa Wafanyabiashara Jijini Mwanza uliofanyika kwa takribani siku mbili kuanzia Juzi Jumatano Agost 20 hadi jana Alhamisi 21, umefikia tamati kufuatia kikao baina ya Wafanyabiashara hao na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.

Kwa takribani kutwa nzima ya jana kulikuwa na vuta nikute katika Kikao cha Jumuia ya wafanyabiashara Mkoani Mwanza na Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, ambapo kikao hicho kilichohitimishwa saa tatu usiku jana kiliadhimia kusitisha mgomo ulioanzishwa na wafanyabiashara hao baada ya kukubaliana kumalizwa kwa kero zilizokuwa zinalalamikiwa na wafanyabiashara hao.
Miongoni mwa Kero zilizokuwa zinalalamikiwa na Wafanyabiashara Jijini Mwanza ni pamoja na Manyanyaso kutoka kwa mgambo wa Jiji, kodi za Taka na Viwango vya leseni wanavyotozwa na Halmashauri ya jiji la Mwanza kuwa kubwa na isiyozingatia usawa sanjari na kupuuzwa na Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, ambapo kikao cha jana kiliadhimia kuondoa kero hizo zote.
Akitoa taarifa ya Kikao hicho kilichofanyika jana katika Ukumbi wa Jiji la Mwanza, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Mkoani Mwanza, Christopher Wambura amesema kuwa kero zote zilizokuwa zikilalamikiwa na wafanyabiashara Mkoani Mwanza sasa zimetafutiwa ufumbuzi.

“Kero zote tulizokuwa tunazilalamikia tumekubaliana ziondolewe ikiwa ni pamoja na kuondoa usumbufu unosababishwa na Mgambo wa jiji kuwakamata wafanyabiashara wanapokuwa wanashusha mizigo yao sanjari na kero zote tulizokuwa tukizilalamikia. Hivyo wafanyabiashara waendelee na shughuli zao kama kawaida” Alisema Wambura.
Maduka Yamefunguliwa na biashara inaendelea kama kawaida.
Wakati hayo yakijiri, duru za habari zinazidi kuzagaa kwamba, migomo ya wafanyabiashara inayoibuka mara kwa mara Jijini Mwanza inahatarija ajira ya Mkurugenzi wa Jiji hilo Mh.Halifa Hida.

“Hii Migogoro mnayoibuka nayo nyie wafanyabiashara unajua inahatarisha ajira ya huyu Mkurugenzi. Kiukweli kama mtaendelea hivi nina wasiwasi na ajira yake maana itaonekana kama jiji hili limemshinda” Alisikika akiongea mmoja wa wajumbe waliohudhuria kikao cha wafanyabiashara hao  kilichofanyika jana.
Na Mhariri: Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.