LIVE STREAM ADS

Header Ads

GIZA NENE MGOMO WA WAFANYABIASHARA JIJINI MWANZA.

Mgomo huo ulianza jana Jumatano Agost 20 na umeendelea leo Alhamisi Agost 2 ikiwa ni siku ya Pili.
Mgomo wa Wafanyabiashara Jijini Mwanza leo umeingia katika Siku yake ya Pili huku Juhudi za kuhakikisha kuwa Mgomo huo unafikia tamati zikiwa zinaendelea ambapo mapema hii leo viongozi wa Jumuia ya Wafanyabiashara Mkoani Mwanza, wamekutana na Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa ajili ya Kutafuta suluhu ya Mgomo huo.

Wakati Mgomo huo Ukiendelea hii leo, Tayari kuna stofahamu miongoni mwa Wafanyabiashara wa Maduka Jijini Mwanza, ambapo miongoni mwao wapo wanaounga mkono uwepo wa Mgomo huo, huku baadhi yao wakiwa hawaungi Mkono Mgomo huo na hivyo kuonekana wakifungua Maduka yao japo kwa tahadhari.
Mapema hii leo asilimia kubwa ya Maduka yalikuwa yamefungwa Jijini Mwanza, huku baadhi ya maduka yakiwa yamefunguliwa nusu milango kutokana na kuhofia usalama wa maduka hayo kwa kuwa baadhi ya wafanyabiashara wasiounga Mkono Mgomo huo wanahofu ya kufungua maduka yao kutokana na vitisho kutoka kwa baadhi yawafanyabiashara kuwashinikiza wafunge maduka yao.

Wakati hali hiyo ikiendelea, gari la matangazo la Halmashauri ya Jiji la Mwanza lilikuwa likizunguka katika Mitaa yote ya Katikati ya Jiji la Mwanza likiwataarifu wafanyabiashara kufungua maduka yao na kutohofia usalama wao kwa kuwa jeshi la polisi limejipanga ili kuhakikisha kuwa wanafanya shughuli zao bila wasiwasi.
Wakati huo huo, Kikao kati ya Viongozi wa Jumuia ya Wafanyabiashara Mkoani Mwanza na Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kimeendelea na Mazungumzo yake, japo hadi tunaingia mitamboni majira ya saa nane Mchana hakukuwa na taarifa yoyote ya matumaini kutoka ndani ya kikao hicho ambacho kimedumu kwa muda mrefu.

Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji Mwanza huku ikiaminika kuwa Murugenzi wa Jiji la Mwanza Mh.Halifa Hida amekubali kujumuika katika kikao hicho baada ya malalamiko ya Muda mrefu kuwa Mkurugenzi huo amekuwa akipuuzia ombi la Wafanyabiashara Mkoani Mwanza la kukutana nao kwa ajili kuzungumzia kero zinazowakabiri.
Miongoni mwa Kero zinazolalamikiwa na Wafanyabiashara wa Mkoani Mwanza si tena Matumizi ya Mashine za EFD’s pekee, bali ni pamoja na Manyanyaso kutoka kwa mgambo wa Jiji, kodi za Taka na Viwango vya leseni wanavyotozwa na Halmashauri ya jiji la Mwanza kuwa kubwa na isiyozingatia usawa huku ndani yake zikiwa zimetaliwa na mazingira ya rushwa sanjari na kupuuzwa na Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Wanahabari waliokuwa wamefika ili kujua kinachoendela kuhusiana na Kikao cha kutafuta suluhu ya Mgomo huo walikuwa wakilalamika kwa kile walichokiitwa kupuzwa na Afisa Uhusiano wa Jiji la Mwanza Joseph Mlinzi ambae alikuwa na Mwongozo mzima wa Kikao hicho na hivyo kulalamika kutokana na kukaa muda mrefu nje ya Ukumbi bila kupewa maelekezo yoyote na hata walipotaka kuingia ndani ya Kikao hicho walizuiliwa na Afisa Uhusiano huyo bila kupewa Maelekezo yoyote ya Msingi mbali na kuambiwa “subirini tutawaita”.
Pengine Kikao hicho kinachoendelea Katika Ukumbi wa Jiji la Mwanza kitaweza kuja na muafaka mwema na hivyo kusitisha Mgomo huo ambao kiukweli umesababisha adha kubwa Jijini Mwanza, hasa ikizingatiwa kwamba Jiji la Mwanza ni Kitovu cha kibiashara katika Ukanda wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo tayari kuna malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara waliotoka Mikoani kwa ajili ya kufuata bidhaa mbalimbali Jijini Mwanza.
Baadhi ya Viongozi wa Jumuia ya Wafanyabiashara akiwemo Christopher Wambura (katikati) Wakitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari wakiwataka kuwa wavumilivu wakati Kikao Kikiendele katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza hii leo. AHSANTE KWA KUTEMBELEA MTANZANIA MEDIA. TUPO KWA AJILI YAKO.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.