LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI 72 MKOANI MWANZA YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 23.

Diana Rwechungura ambae ni Mratibu wa Mwenge wa Uhuru Mkoani Mwanza akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari hii leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Jumla ya Miradi ya Maendeleo 72 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 23 na Milioni 32 inatarajiwa kuzinduliwa Mkoani Mwanza na Mwenge wa Uhuru, ambao unaotarajia kupokelewa kesho katika Wilaya ya Kwimba kabla ya kuendelea na Mbio zake katika Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mwanza.

Hayo yamebainishwa hii leo na
Diana Rwuchengura ambae ni Mratibu wa Mwenge Mkoa wa Mwanza, wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya ujio wa Mwenge huo Mkoani Mwanza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Rwechungura amesema kuwa Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu katika Mkoa wa Mwanza utazindua na Kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya Afya, Kilimo, Uvuvi, Ufugaji, Maji pamoja na Miradi ya Hifadhi ya Mazingira.

“Ndugu wanahabari, mwenge wa Uhuru kwa Mwaka huu, katika Mkoa wa Mwanza utazindua Miradi 72 yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 23,032,780,930. Thamani hii inatokana na Michango ya wananchi shilingi bilioni 2,954,601,360, Serikali kuu bilioni 9,579,458,674, Michango ya Halmashauri bilioni 2,326,173,940 na Michango ya wahisani bilioni 8,172,546,956” Alisema na Kuongeza…

“Ndugu wanahabari, mchanganuo wa miradi hiyo ni kama ifuatavyo, jumla ya miradi 20 yenye thamani ya shilingi bilioni 10,854,827,825 itawekewa mawe ya msingi, miradi 31 yenye thamani ya shilingi bilioni 2,995,339,360 itazinduliwa, miradi 18 yenye thamani ya shilingi bilioni 8,804,132,745 itafunguliwa na miradi mitatu yenye thamani ya milioni 378,481,000 itakaguliwa…”.
Pesha Moses ambae ni Katibu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Aidha Rwechungura ameongeza kuwa moja ya majukumu ya Mwenge wa Uhuru ni pamoja na kubeba ujumbe mkuu kwa mwaka husika, ambapo ujumbe mkuu kwa mwaka huu ni “Katiba ni Sheria Kuu ya nchi, Jitokeze kupiga kura ya Maoni tupate Katiba Mpya”.

Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Mwanza unatarajiwa kupokelewa kesho Septemba 18 katika Wilaya ya Kwimba na kasha kuendelea na mbio zake katika Wilaya za Magu, Ilemela, Ukerewe, Nyamagana na Misungwi kabla ya kuhitimisha mbio zake Septemba 24 katika Wilaya ya Sengerema ambapo Mwenge huo utakabidhiwa katika Mkoa wa Geita Septemba 25 mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na mbio zake.

Mbali na hayo wanahabari Mkoani Mwanza wamelalamikia kitendo cha Kutojumuishwa katika shughuli za Mwenge huo kwa kile kilichodaiwa kwamba ni bajeti finyu iliyotengwa kwa ajili ya shughuli za Mwenge huo ambapo chombo kimoja cha Runinga ambacho ni cha Serikali ndicho kimejumuishwa katika ziara za mwenge huo Mkoani Mwanza. 

"Sisi tunawashangaa eti mnasema bajeti. Waandishi sisi hatupo kwa ajili ya kulipwa posho. Mnashindwa kutenga gari hata moja kwa ajili ya Waandishi wa Habari, mnasema eti bajeti haitoshi. Nashangaa hicho chombo cha habari mnachosema kwamba mmekichagua kwa ajili ya shughuli hizo za Mwenge hata hapa hakipo. Kiukweli kwa hili mnapaswa kujirekebisha. Alisema mmoja wa Waandishi wa Habari waliofika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kupokea taarifa ya ujio wa Mwenge Mkoani Mwanza.
Diana Rwechungura ambae ni Mratibu wa Mwenge wa Uhuru Mkoani Mwanza (Kushoto) akiwa na William James (Kulia) kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Diana Rwechungura ambae ni Mratibu wa Mwenge wa Uhuru Mkoani Mwanza (Wa kwanza Kushoto) akiwa na William James (Katikati) pamoja na Pesha Moses ambae ni Katibu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (Wa kwanza Kulia)
Waandishi wa Habari.
Waandishi wa Habari.
Waandishi wa Habari.
Waandishi wa Habari.
Hii leo Wanahabari wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya Kupokea taarifa juu ya Ujio wa Mwenge wa Uhuru Mkoani Mwanza.
Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya Habari Jijini Mwanza wakitoka inje ya Ukumbi wa Mikutano katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo.
Waandishi wa Vyombo mbalimbali Jijini Mwanza wakitoka inje ya Ukumbi wa Mikutano katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza baada ya kupokea taarifa ya Ujio wa Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa Kupokelewa Kesho Septemba 18 katika Wilaya ya Kwimba na baadae kuendelea na mbio zake katika Wilaya za Magu, Ilemela, Ukerewe, Nyamagana, na Misungwi na hatimae kuhitimisha Mbio hizo katika Wilaya ya Sengerema Septemba 24 ambapo Sepemba 26 Mwenge huo utakabidhiwa katika Mkoa wa Geita na kuendelea na Mbio zake.

No comments:

Powered by Blogger.