BABA AMSABABISHIA MWANAE KIFO KUTOKANA NA KIPIGO JIJINI MWANZA. AMFICHA MWINGINE NDANI AKIWA NA MAJERAHA MAKUBWA.
Mwanaume mmoja Mkazi wa Jijini Mwanza
anatuhumiwa kwa kosa la kusababisha Mauaji ya Mtoto wake, huku mtoto mwingine nae
akiwa katika hali mbaya ya majeraha baada ya watoto hao kwa nyakati tofauti
kudaiwa kupigwa na mwanaume huo.
Tukio hilo
limetokea katika Mtaa wa Mwembeni A katika Kata ya Pamba iliyoyopo Wilaya ya
Nyamagana Jijini Mwanza, ambapo mwanaume huyo ambae ni mzazi wa watoto hao
anadaiwa kuwa alikuwa na desturi ya kuwapiga watoto hao mara kwa mara kwa madai
kwamba si damu yake.
Katika tukio
la Kwanza Mwanaume huo ambae ametajwa kwa jina la Mwita au Yusuph anadaiwa kumpiga
mtoto wake wa kambo na kumsababishia majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili
wake hali iliyosababisha mtoto huyo kupoteza maisha akiwa katika Hospitali ya
Mkoa wa Mwanza Sekour Toure baada ya kumficha mtoto huo nyumbani kwa siku
kadhaa bila matibabu.
Mtoto
aliefariki kutokana na majeraha yaliyotokana na kipigo kutoka kwa mwaume huyo
anafahamika kwa jina la Wambura Yusuph mwenye umri wa miaka miwili, ambae
amefariki hii leo akiwa katika Hospital ya Sekour Toure akipatiwa matibabu.
Majirani wakiwa na Majonzi tele baada ya Kupata taarifa ya jirani mwenzao kumpiga mtoto wake hali iliyosabanisha mtoto huyo kufikwa na umauti kutokana na kipigo hicho. |
Katika tukio
la pili Mwanaume huyo pia, anadaiwa kumpiga mtoto wake mwingine hadi kufikia
hatua ya kumchoma moto. Mtoto huyo anafahamika kwa jina la Baraka Mussa
mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu na kumsababishia majeraha makubwa katika sehemu za
mwili wake hususani magotini na kasha kumficha ndani huku na kuendelea kumtibu
kiholela.
Baada ya
kupata taarifa hizo, Shirika la kutetea haki za Watoto la Foundation Karibu
Tanzania lililopo Mkoani Mwanza kupitia kwa Johanes Emmanuel ambae ni Afisa
Ustawi wa Shirika hilo kwa kushirikiana na viongozi wa Mtaa huo waliweza kufika
nyumbani kwa Mwanaume huyo kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria sanjari na
usaidizi wa mtoto aliekuwa amefichwa ndani akiuguza majeraha.
Hatimae
mwanaume huyo alifika nyumbani na kutakiwa kuambatana na viongozi wake wa mtaa
kwenda katika kituo cha polisi kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili, lakini
juhudi hizo hazikuweza kuzaa matunda kwani mwanaume huo alifanikiwa kutoroka na
kutokomea kusikojulikana.
Baada ya
Mwanaume huo kutoroka, Viongozi wa Mtaa huo wa Mwembeni A waliamua kuondoka na
Wake za Mwanaume huyo, ambapo Mke mmoja aliefahamika kwa jina la Christina
Mussa (21) ndie mwanae Baraka Mussa (1) alikuwa amefichwa ndani akiwa na
majeraha huku Nyangi Yusuph (23) akiwa ndie mwanae Wambura Yusuph (2) amefikwa
na umauti.
Afisa Mtendaji Mtaa wa Mwembeni A Prisca Evarist (Kushoto) akiwa na baadhi ya Wakazi wa Mtaa huo nyumbani kwa mwanaume anaedaiwa kutenda ukatili kwa watoto. |
Hadi
tunakwenda mitamboni Wanawake hao walikuwa wamefikishwa katika Kituo Kikuu cha
Polisi Nyamagana kwa ajili ya kutoa maelezo juu ya matukio hayo, ambapo kwa
upande wa majirani wamewatupia lawama wanawake hao kutokana na kuyafumbia macho
matukio hayo. Na hapa mama wa Mtoto aliechomwa moto anaeleza jinsi ilivyo kuwa.
Kwa pamoja
Seleman Nasoro ambae ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwembeni A, Maria Thomas ambae ni Balozi wa Mtaa Mwembeni A pamoja na Prisca
Evarist ambae ni Afisa Mtendaji wa Mtaa huo wa Mwembeni A wamelaani kitendo
kilichofanywa na Mwanaume huo ambapo wametoa rai kwa wanajamii kutokaa kimya
pindi wanapoona matukio ya kikatili katika maeneo yao.
Majirani nao
wakaelezea kusikitishwa kwao na Kitendo cha Mwanaume huyo kuwaadhibu watoto
wake kikatili huku wakiwatupia lawama wakielekeza lawama kwa wake wote wawili
wa mwanaume huyo kwa kitendo cha kukaa kimya bila kulipoti vitendo vya kikatili
vilivyokuwa vikifanywa na mwanaume huo.
Awali
akizungumza juu ya Matukio mbalimbali ya Kikatili wanayotendewa watoto katika
Jamii, Abimeleck Richard ambae ni Mwezeshaji na Mwanasheria kutoka Shirika la kutetea
haki za watoto lililopo Mkoani Mwanza la Foundation Karibu Tannzania ameishauri
jamii kuwa tayari kuchukia vitendo vya kikatili vinavyotokea katika jamii.
Christina Mussa ambae ni Mama wa Mtoto Baraka Mussa ambae ameunguzwa na kufichwa ndani kwa muda mrefu bila matibabu. |
Nyangi Yusuph (23) ambae mwanae Wambura Yusuph (2) amefariki baada ya kuuguza kwa siku kadhaa majeraha yanayodaiwa kusababishwa na kipigo kutoka kwa baba yake wa kambo. |
Nyangi Yusuph (23) (kushoto) ambae mwanae Wambura Yusuph (2) amefariki baada ya kuuguza kwa siku kadhaa majeraha yanayodaiwa kusababishwa na kipigo kutoka kwa baba yake wa kambo. |
Mtoto Yusuph (mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu) akiwa katika hali ya majeraha baada ya kufichwa ndani kwa siku kadhaa. |
No comments: