LIVE STREAM ADS

Header Ads

PROMOSHENI YA COKE STUDIO YAZINDULIWA RASMI KANDA YA ZIWA.

Ile Promosheni kubwa kabisa Barani Afrika inayofahamika kwa jina la Coke Studio ambayo inaendeshwa na Kampuni ya Cocacola imezinduliwa Rasmi Katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa. Kampeni hiyo ya Coke Studio inamuwezesha Mtumiaji wa Soda za Cocacola kujishindia muda wa Maongezi wa dakika 5, SMS pamoja na vifurushi vya Internet kwa watumiaji wa mtandao wa Vodacom. Unachotakiwa kufanya ni kununua soda za Cocacola zenye kizibo cha njano na unatuma namba zilizoandikwa katika kizibo hicho kwenda namba 15441.
Marco Masaka (Aliechomekea Tshirt) amabe ni Meneja Masoko Kanda ya Ziwa kutoka Kampuni ya Nyanza Bottling inayotengeze inayotengeneza Vinywaji jamii ya Cocacola akifurahia pamoja na wafanyakazi wengine wa Kampuni hiyo hii leo baada ya Uzinduzi wa Promosheni ya Coke Studio katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Shangwe kwa Wafanyakazi wa Nyanza Bottling Company zikiendelea mara baada ya Uzinduzi wa Promosheni ya Coke Studio Kanda ya Ziwa. Baada ya Promosheni hiyo kuzindulia hii leo, itafuatiwa Show kubwa kabisa ya Coke Studio Mkoani Mwanza jumapili ya Septemba 21 katika Uwanja wa Furahisha ambapo Jukwaani watakuwepo wasanii mbalimbali wakiongozwa na Izzo Busness, Madee pamoja na Shaa.
Marco Masaka ambae ni Meneja Masoko kutoka Nyanza Bottling Company ambao ni watengenezaji wa Vinywaji jamii ya Cocacola akizungumza katika Uzinduzi wa Promosheni hiyo ya Coce Studio. Show ya Coke Studio pia hurushwa hewani kila jumamosi saa tatu jioni na kituo cha Runinga cha TBC 1.
Wafanyakazi wa Nyanza Bottling Company wakiwa wameshirikilia soda za Cocacola ambazo zina muda wa maongezi wa dakika tano, SMS pamoja na Vifurushi vya Internet. Na hii ni kwa kila soda ya Cocacola yenye Kizibo cha Njano. Unachotakiwa kufanya ni kununua soda ya Cocacola yenye kizibo cha njano, kisha unaandika namba zilizo katika kizibo na kuzituma kwenda namba 15441 ambao promosheni hii ni kwa watumiaji wa mtandao wa Vodacom Pekee.
Burudani mbalimbali pia zilikuwepo katika Uzinduzi huo wa Promosheni ya Coke Studio Kanda ya Ziwa uliofanyika hii leo katika viwanja vilivyopo katika Kiwanda cha Nyanza Bottling Company maeneo ya Igoma Jijini Mwanza.
Utakukmbuka kwamba Coke Studio ni Show ambayo inawakutanisha wasanii na waandaaji wa muziki kutoka Barani Afrika na inarushwa katika Vituo vya Runinga ikiwemo TBC 1 kila jumamosi saa tatu usiku kwa Tanzania. Wasanii wa Coke Studi wanaotoka Tanzania ni Diamond Platnum, Shaa na Lady Jaydee.
Burudani zilikuwa si mchezo. Na huu ulikuwa ni mwanzo tu, Burudani zaidi itapigwa siku ya Jumapili katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza. Hapa Madee, pale Shaa na Kule Izzo Busness.
Wananchi na wapenzi wa Soda za Cocacola wajionea burudani iliyokuwa ikitolewa hii leo katika Viwanja vya Nyanza Bottling Company ikiwa ni katika Uzinduzi wa Promosheni ya Coke Studio ambapo watumiaji wa Mtandao wa Vodacom wataweza kujishindia muda wa maongezi wa dakika tano, sms na vifurushi vya Internet pindi wanaponunua soda za Cocacola zenye vizibo vya njano na kisha kutuma namba zilizopo katika vizibo kwenda namba 15441.
Msafara wa ukiwa na Soda za Cocacola kwa ajili yako mpendwa mtumiaji wa Soda za Cocacola.
Tunashukuru kwa kuendelea kuburudika na Habari/ Picha kutoka Mtanzaniamedia Blog. Endelea kutumia Soda za Cocacola ili kujishindia Muda wa Maongezi, sms na vifurushi vya Internet. Usikose kujongea katika Uwanja wa Furahisha siku ya Jumapili ya Septemba 21 ili kuburudika na Showz za Coke Studio ambapo wasanii mbalimbali wakiongozwa na Madee, Shaa na Izzo Busness watakuwepo.

No comments:

Powered by Blogger.