LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANAFUNZI LUMALA SEKONDARI WAFANYA ZIARA YA KIMASOMO NYANZA BOTTLING COMPANY.

Wanafunzi wa Kidato cha Tatu kutoka Shule ya Sekondari Lumala iliyopo Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza wakiwa na Mwalimu wao wa Somo la Biashara anaejulikana kama Mwl.Rogers Ntonda (Wa kwanza Kulia) baada ya hii leo kutembe Kiwanda cha Nyanza Bottling Company kilichopo Igoma Jijini Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kimasomo.
Wanafunzi hawa wameelezea kufurahishwa kwao na Ziara hii ambayo ni ya Kimasomo katika Kiwanda cha Nyanza Bottling Company ambacho kinazalisha vinywaji mbalimbali ikiwemo Cocacola kwa ajili ya kujifunza zaidi juu ya masuala ya uzalishaji. Baadhi yao wamevutiwa na kuenlezea ndoto zao za kuwa na hamu ya kumiliki viwanda vyao pindi watakapohitimu masomo.
Kutokana na Umhimu wa Ziara kama hii kwa ajili ya wao kujifunza kwa vitendo, wanafunzi hawa wameomba kuwa na ziara za mara kwa mara ambazo zinawapata fursa ya kujifunza zaidi kwa vitendo.
Mwalimu Rogers Tonda ambae ni Mwalimu wa Somo la Biashara Lumala Sekondari ameiambia Mtanzaniamedia Blog kwamba, Ziara za kimasomo kwa wanafunzi inje ya shule zina manufaa makubwa kwa kuwa humwezesha mwanafunzi kujifunza vyema zaidi na kwa vitendo na hivyo kumpa uelewa mpana zaidi mwanafunzi.
Wanafunzi wa Kidato cha Tatu kutoka Lumala Sekondari iliyopo Ilemela Mkoani Mwanza.
Wanafunzi wa Kidato cha Tatu kutoka Lumala Sekondari iliyopo Ilemela Mkoani Mwanza.
Wanafunzi wa Kidato cha Tatu Lumala Sekondari walipofanya ziara ya kimasomo katika Kiwanda cha Nyanza Bottling Company kwa ajili ya kujifunza namna kiwanda hicho kinavyozalisha vinywaji (Soda).
Mtanzaniamedia Blog Inawatakia masomo mema na jiepusheni na Mafataki maana Taifa linawategemea sana hivyo zingatieni Masomo kwa bidii.

No comments:

Powered by Blogger.