LIVE STREAM ADS

Header Ads

PEPSI YAKABIDHI VIFAA VYA BIASHARA KWA WASICHANA WALIOACHA SHULE MKOANI MWANZA.

Picha ya Pamoja baina ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Viongozi wengine akiwemo Meya wa Jiji la Mwanza, Uongozi wa Kiwanda cha Pespi SBC Tanzania, Shirika la EBLI na baadhi ya wanafunzi waliochishwa Masomo Mkoani Mwanza kutokana na sababu mbalimbali ikwemo mimba.
Baadhi ya wasichana walioachisha masomo Mkoani Mwanza kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo Mimba, wamepatiwa Vifaa vya biashara na Kampuni ya Vinywa ya Pepsi SBC Tanzania kwa lengo la kuwasaidia wasichana katika shughuli zao za ujasiriamali.

Takribani wasichana
45 Mkoani Mwanza wamenufaika na Vifaa hivyo ambavyo ni Matoroli na Makasha ya kubebea barafu yaliyotolewa kwa akina dada 25, sanjari na meza pamoja na viti kwa ajili ya akina dada 20 ambao tayari wameanzisha biashara ya mama lishe. 

Akikabidhi vifaa hivyo jana, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, alielezea kufurahishwa na Msaada uliotolewa na Kampuni hiyo ya Vinywaji ya Pepsi SBC Tanzania kwa kuwa utawawezesha wasichana hao kuboresha biashara zao.

“Vifaa hivi ni imani yangu kuwa vitaboresha biashara za akina dada hawa na hivyo kuwaongezea tija katika uendeshaji wa shughuli zao na kuongeza kipato chao kiuchumi”. Alisema Mhandisi Ndikilo.

Katika hatua nyingine Mhandisi Ndikilo amelishukuru Shirika lisilo la Kiserikali Mkoani Mwanza la Education for Better Living (EBLI) ambalo kwa kushirikiana na wadau wengine kama Pespi SBC Tanzania limeadhimia kuwasaidia wasichana walioacha masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo suala la Miamba.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist ndikilo jana akiwakabidhi wasichana waliokatishwa masomo Mkoani Mwanza kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mimba, vifaa vya biashara vilivyotolewa na Kampuni ya kutengeneza vinywaji ya Pepsi SBC Tanzania.



Aidha Mhandisi ndikilo ametoa rai kwa akina dada hao waliopata vitendea kazi hivyo vya biashara kuvitumia kwa manufaa yaliyokusudiwa ili kujiletea maendeleo yao na jamii nzima kwa ujumla.

Kwa upande mwingine Mhandisi Ndikilo pia amewasihi wasihi wananchi wa Mkoa wa Mwanza kuendelea kutoa ushirikiano Mkubwa na Kampuni ya Vinywaji ya Pepsi SBC Tanzania kwa kutumia bidhaa zao kwa wingi ili Kampuni hiyo iendelee kusaidia katika jamii kupitia Mpango wake wa Cooperate Social Responsibility.

Awali pia Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Amina Masenza aliishukuru Kampuni ya Pespi SBC Tanzania kwa Vifaa walivyowapatia wasichana hao, ambapo aliwataka wasichana hao kuvitumia vifaa hivyo kwa manufaa zaidi na kukuza biashara zao na kuepukana na mashindano ya kujiremba sanjari na starehe ili kuweza kusonga mbele kimaendeleo zaidi.                        

Nao baadhi ya Wasichana waliopokea Vifaa hivyo wamesema kuwa vifaa walivyovipokea vitawasaidia katika shughuli zao na hivyo kuwaongezea faida ambayo itawawezesha kuwalea watoto wao vyema ambapo pia wametoa rai kwa wasichana wenzao kuzingatia zaidi elimu na kujiepusha na tamaa za dunia.
Kampuni ya Pepsi SBC imeungana na Shirika lisilo la Kiserikali la Education for Better Living (EBLI)
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiwa amembeba mmoja wa watoto wa Msichana alieachishwa masomo yake kutokana na ujauzito.
Matoroli na Makasha ya kubebea barafu ambayo ni baadhi ya Vifaa vya biashara vilivyotolewa na Kampuni ya Vinywaji ya Pepsi SBC kwa ajili ya wasichana walioachishwa masomo Mkoani Mwanza kuvitumia kwa ajili ya biashara zao za kiujasiriamali.
Matoroli na Makasha ya kubebea barafu ambayo ni baadhi ya Vifaa vya biashara vilivyotolewa na Kampuni ya Vinywaji ya Pepsi SBC kwa ajili ya wasichana walioachishwa masomo Mkoani Mwanza kuvitumia kwa ajili ya biashara zao za kiujasiriamali.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo akipokelewa jana baada ya kuingia katika viunga vya Kiwanda cha Pepsi SBC igoma Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akizungumza jana kabla ya kukabidhi vifaa vya Biashara kwa ajili ya wasichana walioachishwa masomo yao Mkoani Mwanza. Vifaa hivyo vilitolewa na Kampuni ya Pespi SBC.
Wanahabari wakiwa katika majukumu yao ya kunasa matukio.
Baadhi ya wasichana walioachishwa masomo Mkoani Mwanza kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupachikwa Mimba.
Baadhi ya viongozi na Watumishi wa Kampuni ya Vinywaji ya Pepsi SBC.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kiwanda cha Pepsi SBC.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist ndikilo (Kulia aliekaa) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Amina Masenza (Kushoto aliekaa).
Pesha Moses ambae ni Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Baadhi ya wasichana walioachishwa masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo suala la mimba Mkoani Mwanza.
Ahsante kwa kutembelea Mtanzaniamedia Blog. Endelea kuwa nasi huku ukitumia Vinywaji jamii ya Pepsi ili kuiwezesha kampuni hii kurudisha katika jamii kile inachokipata.

No comments:

Powered by Blogger.