LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKOLANI MABINGWA WAPYA PEPSI KOMBE LA MEYA 2014.

Kikosi cha Timu ya Mkolani FC Kutoka Jijini Mwanza mara baada ya Kuibuka Mabingwa wapya wa Pepsi Kombe la Meya kwa Kuitungua Timu ya Mirongo ya Jijini Mwanza kwa bao 2-1. Mchezo wa Fainali katika Michuano hiyo ulipigwa jana katika dimba la Nyamagana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Serikali na Shirikisho la Soka nchini TFF sanjari na Mashabiki kujitokeza kwa wingi. Magoli ya Timu ya Mkolani yalifungwa na
Mashaka Damalo goli la kwanza katika dakika 49 kipindi cha pili na Paul Godfrey akatundika bao la pili katika dakika 76 kipindi cha pili. Bao la Kufutia machozi kwa timu ya Mirongo lilipatikana katika dakika ya 83 baada ya beki wa Timu ya Mkolani Meck Lymo Kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa Mpira.
Mgeni Rasmi ambae ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo (Mwenye Koti) akiwakabidhi Kombe wachezaji wa Timu ya Mkolani baada ya Kuibuka Mabingwa wa Pepsi Kombe la Meya mwaka 2014. Mbali na Kombe, Mshindi wa Kwanza katika Michuano hiyo alijipatia shilingi Milioni moja na nusu, medali ya dhahabu na bajaji ya kisasa ya mizigo yenye thamani ya shilingi milioni 4.5
Wachezaji wa Timu ya Mkolani ambao ni mabingwa wapya wa Michuano ya Pepsi Kombe la Meya wakipita Jukwaani Kukabidhiwa Zawadi zao. Wa kwanza Kulia ni Muasisi wa Michuano hiyo Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza na Diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) akinong'onezana jambo na mchezaji wa Timu ya Mkolani.
Kikosi cha Timu ya Mkolani FC.
Paul Godfrey ambae ni Mfungaji bora wa Michuano ya Pepsi Kombe la Meya ambapo hadi michuano inamalizika alikuwa ametupia amecheka na nyavu mara Tisa. Amejishindia kitita cha Shilingi Laki Mbili na Kiatu Kiatu cha dhahabu.
Wachezaji wa Timu ya Mirongo FC wakipokea zawadi baada ya kuibuka Washindi wa Pili katika Michuano ya Pepsi Kombe la Meya iliyofikia tamati jana katika Uwanja Mkongwe wa Nyamagana. Mirongo iliingia fainali na Timu ya Mkolani na katika mechi ya Fainali ikatundikwa bao 2-1.
Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Joas Selestine akiwakabidhi Wachezaji wa Timu ya Mirongo Kombe baada ya Kuibuka Washindi wa Pili katika Michuano ya Pepsi Kombe la Meya mwaka 2014. Mbali na Kombe, Mshindi wa Pili pia alijinyakulia Kitita cha Shilingi Milioni Mbili na Medali ya Fedha.
Diwani wa Kata ya Mirongo akifurahi na Kombe ambalo timu yake ya Mirongo imejishindia baada ya kuibuka Washindi wa Pili katika Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014.
Wachezaji wa Timu ya Sokoni FC ambao ni Washindi wa Tatu wa Tatu wa Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 wakipokea Zawadi zao. Timu ya Sokoni FC iliibuka Mshindi wa Tatu baada ya kuitandika Timu ya Mnadani FC kwa bao 3-0 katika mechi ilichezwa jana katika Uwanja wa Nyamagana majira ya saa nane kabla ya mchezo wa Fainali. Mshindi wa Tatu katika Michuano hiyo amejinyakulia kitita cha shilingi Milioni Moja, Medali ya Shaba pamoja na Kombe dogo.
Wachezaji wa Sokoni FC Wakifurahia Kombe walilojishindia baada ya kuibuka washindi wa Tatu katika Michuano ya Pepsi Kombe la Meya. Kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Halifa Hida akifungua bahasha yenye Kitita cha Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya Kuwakabidhi wachezaji wa timu hiyo.
David Albert (mwenye jezi) ambae ni Mwamuzi bora wa Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014. Mwamuzi bora katika Michuano hiyo amejishindia fedha taslimu shilingi Laki Mbili. Michuano hii ilichezeshwa na Waamuzi kutoka Shule ya Vipaji ya Alliance ya Jijini Mwanza.
David Albert akifurahia kitita cha Shilingi Laki Mbili baada ya kuibuka kuwa Mwamuzi bora wa Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014. Albert pia ndie aliechezesha Mechi ya Fainali na kuonekana kuimudu vyema mechi hiyo.
Nicolas Coertz ambae ni Meneja wa Kampuni ya Vinywaji ya Pepsi SBC Tanzania Mkoani Mwanza.
Muasisi wa Michuano ya Pepsi Kombe la Meya ambae ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza na Diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslauns Shing'ongo Mabula.
Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Joas Selestine akizungumza jana katika Uwanja wa Nyamagana katika Fainali za Michuano ya Soka ya Pepsi Kombe la Meya 2014. Selestine aliwahakikishia wapenda soka na wa Jiji la Mwanza kwamba, Mwakani Michuano ya Pepsi Kombe la Meya lazima ifanyike katika Uwanja wa Nyamagana huku ukiwa tayari na Nyasi mbandia baada ya zoezi la uwekaji wa Nyasi mbandia katika Uwanja huo kuonekana kuchukua muda mrefu licha ya mara kwa mara kuelezwa kwamba taratibu za kuuwekea nyasi mbandia Uwanja huo zimekwisha kamilika.
Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Joas Selestine (Kushoto) akizungumza katika Fainali hizo za Pepsi Kombe la Meya. Kulia ni Muasisi wa Michuano hiyo Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza na Diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) Stanslauns Shing'ong'o Mabula.
Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Joas Selestine (Kulia) akizungumza katika Fainali za Pepsi Kombe la Meya jana. Kushoto (Mwenye Tshirt) ni Balozi wa Habari Pepsi Kombe la Meya Albert Gsengo akifuatiwa na Mnasa matukio kutoka Mwanza Satelite Tv.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo (Katikati) akizungumza katika Fainali hizo za Pepsi Kombe la Meya 2014. Wa kwanza Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoani Mwanza (MZFA) Jackson Manji Songora.
Makombe yakiwa katika hali tulizo kabla ya Kukabidhiwa kwa Washindi.
Maua a.k.a Warembo waliokuwa wakihakikisha kwamba Kombe linakuwa katika hali nzuri na ya kuvutia kama wao wenyewe walivyo.
Baadhi ya Mashabiki waliojitokeza katika Kushuhudia Fainali za Pepsi Kombe la Meya zilizochezwa jana katika Uwanja Mkongwe wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Baadhi ya Mashabiki wakiwa Jukwaa kuu wakifuatiria kwa Umakini Fainali za Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014 ambapo Timu ya Mkolani waliibuka Mabingwa wapya baada ya Kuilaza Timu ya Mirongo kwa bao 2-1. Mwaka jana Mabingwa wa Michuano hiyo walikuwa ni Isamilo FC lakini mwaka huu hali ilikuwa mbaya kwao na kujikuta wakitolewa katika michuano hiyo mapema kabisa. Michuano hiyo ilianza kutimua mbio zake Agost Mbili mwaka huu na imefikia tamati jana Septemba 20 ambapo ilishirikisha Jumla ya Timu 22.

No comments:

Powered by Blogger.