LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI WAFURAHISHWA NA HUDUMA ZA AFYA ZINAZOTOLEWA NA KITUO CHA AFYA AGA KHAN MKOANI MWANZA.


Wananchi Mkoani Mwanza wameelezea kufurahishwa kwao na huduma za Afya zinazotolewa mara kwa mara na kituo cha Afya Aga Khan katika maeneo mbalimbali, na hivyo kuwarahisishia upatikanaji wa huduma za Matibabu.

Wananchi hao
waliyasema hayo jana katika Uwanja wa Magomeni ulioko Kata ya Kirumba Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wakati wakizungumza nasi juu ya mwitikio wa wananchi kujitokeza kupima Afya zao.

Walisema mwitikio wa wananchi Mkoani Mwanza katika kujitokeza kupima afya zao bado ni mdogo, jambo ambalo walisema kuwa linasababishwa na kipato duni kwa wananchi hali ambayo walisema inahatarisha maisha yao kwa kuwa baadhi ya wananchi wamejenga desturi ya kujinunulia dawa mitaani na kuzitumia kabla ya kupima kwa minajiri ya kukwepa gharama za matibabu.

Aidha waliushukuru uongozi wa Kituo cha Afya Aga Khan ambacho kimekuwa na desturi ya kutoa bure huduma za upimaji sanjari na ushauri na saha juu ya masuala mbalimbali ya kiafya kwa wananchi.

Kituo cha Afya Aga Khan kinaendesha huduma ya Upimaji sanjari na Ushauri na Saha juu ya masuala mbalimbali ya afya kwa wananchi katika Uwanja wa Magomeni ulioko Kirumba Wilayani Ilemela ambapo Kampeni ya Mwanamke na Uchumi inafanyika.

Kampeni hiyo ambayo inadumu Mkoani Mwanza kwa Siku mbili ilianza jana Septemba nne na inatamatishwa leo Septemba tano ambapo jumla ya wanawake wajasiriamali 500 kutoka Wilaya za Magu, Ilemela na Nyamagana jana walikutana kwa ajili ya kupata elimu ya masuala mbalimbali ya Ujasiriamali huku wengine 500 leo nao wakitarajiwa kupata elimu hiyo.

Kampeni hiyo ya Mwanamke na Uchumi imeandaliwa na Taasisi ya Angels Moment kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto pamoja na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), ambapo imelenga kuwapatia wanawake elimu ya Ujasiriamali kulingana na fursa zilizopo katika mazingira yao.

Neema Malima ambae ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Angels Moment iliyoandaa Kampeni hiyo ya Mwanamke na Uchumi, amebainisha baadhi ya mafunzo yanayotolewa ni pamoja na ujasiriamali na fursa zinazomzunguka mwanamke kabla ya kuanzisha biashara pamoja na usimamizi binafsi wa fedha na uwekaji wa akiba.

Mafunzo mengine ni pamoja na Afya bora kwa mwanamke na Uchumi imara ambapo wanawake wanapewa elimu katika kutatua changamoto za magonjwa ya wanawake ambayo ni kikwazo katika shughuli zao.

Kwa Mkoa wa Mwanza Kampeni hiyo ya Mwanamke na Uchumi imewajumuisha Wanawake wajasiriamali kutoka Wilaya za Magu, Ilemela na Nyamagana huku pia Mikoa ya Kigoma, Tanga, Ruvuma, Dodoma, Pwana na Lindi ikitarajiwa kunufaika na Kampeni hiyo hapa nchini.

Akizungmza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amina Masenza ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela amewataka wanawake waliohudhuria katika Kampeni hiyo kuwa chachu ya Maendeleo kwa kufanya biashara endelevu na yenye tija kwa kujiwekea akiba sanjari na kutumia faida faida ya biashara yao katika kujiongezea mtaji.


Amewasihi zaidi kutumia daftari katika kutunza taarifa zao kwa kuwa biashara bila daftari huisha bila taarifa huku pia akiwasihi akinamama hao waliohudhuria katika Kampeni hiyo ya Mwanamke na Uchumi Mkoani Mwanza kujenga tabia ya kupima afya mara kwa mara wao na familia zao kwa lengo la kutambua afya zao jambo litakalowasaidia wao na familia zao katika kumudu shughuli zao vyema.

Aidha ametoa wito kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza kuhakikisha kwamba Maafisa Maendeleo ya Jamii wanatumika ipasavyo katika kuwahudumia wananchi ambapo amewasihi akina mama kufika katika ofisi za Maafisa Maendeleo ya Jamii walio katika Halmashauri zao kwa lengo la kupata huduma kwa kuwa Maafisa Maendeleo hao wameajiriwa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.

Katika Kuhitimisha hotuba yake aliyoisoma kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Masenza ametoa tahadhari kwa akina mama kujiepusha na vitendo viovu ambavyo vimekuwa vikitendeka katika maeneo mbalimbali hususani kwa wavuvi ambapo wanawake wamekuwa wakitumika kingoko katika kujipatia mahitaji yao kupitia mfumo uitwao hamsini kwa hamsini ambapo mwanamke hulipia nusu ya gharama ya mahitaji yake na nusu nyingine inayobaki mwanamke huilipia kwa njia ya ngono.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Amina Masenza (Mwenye Miwani) akisaini kitabu cha mahudhurio katika mabanda yaliyopo Magomeni Kirumba inakofanyika Kampeni ya Mwanamke na Uchumi.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana akikagua bidhaa zilizo katika mabanda ya Wanawake wajasiriamali.
Bidhaa za Akina Mama Wajasiriamali.
Bidhaa za Akina Mama Wajasiriamali.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL Altaf Mansoor (Kulia) akiangalia Majarida katika banda la Mamlaka ya Mfuko wa udhibiti Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (SSRA). Kushoto ni Sarah Kibonde Msika ambae ni Afisa Mawasiliano, Promosheni na Uhamasishaji kutoka SSRA.
"Hapa wanafurahia ngoma kutoka Bujora"
Kwa Upande wake Paul Manyika ambae ni Afisa Viwango kutoka Shirika la Viwango nchini TBS (Katikati) akiwa na Stella Mrosso ambae ni Mkuu wa Maabala ya Chakula TBS (Kulia). Wa kwanza kutosho ni Mwanahabari kutoka Star Tv.
Ngoma kutoka Katika Kundi la Bujora ilikuwa ikitumbuiza pia.
"Hano ndangee Mkunguu Maghena ndaleeee x4"
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.