LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAONYESHO YA BIASHARA YA AFRIKA MASHARIKI YAFUNGULIWA RASMI JIJINI MWANZA.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania George Owio ameipongeza Chemba ya Wafanyabiashara za Viwanda na Kilimo TCCIA kwa juhudi za kufanikisha Maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki kwa mara ya Tisa mwaka huu.

Owio aliyasema hayo jana Mkoani Mwanza katika ufunguzi rasmi wa Maonyesho hayo ya biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea katika Uwanja Mkongwe wa Nyamagana ambapo pia aliitaka TCCIA kuendeleza juhudi hizo.
Kwa Upande wake Peter Chisawillo ambae ni Rais wa TCCIA aliwataka Wafanyabiashara wa Afrika Mashariki kuzidisha ubora katika uzalishaji wao ili kushindana na soko la Kimataifa huku Elibariki Mmari ambae ni Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza akiwataka wafanyabiasharakuendelea kushiriki kwa wingi katika maonyesho hayo kwa lengo la kutangaza biashara zao.
Maonyesho hayo ya Biashara ya Afrika Mashariki yalianza tangu tarehe 29 mwezi Agost na yamefunguliwa rasmi hii leo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ambapi yanatarajiwa kufungwa rasmi Septemba Saba mwaka huu.
"HATOKI MTU HAPA, AIRTEL YATOSHA" Ndivyo Mtanzania Media ilivyokaribishwa katika banda la Airtel.
Simu bomba na Kali zinazopatikana banda la Airtel katika Maonyesho hayo.
Balozi wa China nchini Tanzania Li Xuhang akisaini katika kitabu cha mahudhurio wakati akitembea kukagua mabanda ya maonyesho.
Balozi wa China nchini Tanzania Li Xuhang (Katikati) akifurahia ubunifu wa kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa kutumia ngozi. Wa kwanza kushoto ni Elibariki Mmari ambae ni Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza.
Hili ni Banda la Top Manyota na Kazi Moto ambalo linashughulika na Tiba Asilia ya Binadamu sanjari na Ushauri na Saha. Dawa zao zinatibu magonjwa mbalimbali. Fika katika Viwanja vya Nyamagana ili kuonana nao au  Wasiliana nao kwa nambari 0752 308 447 AU 0786 547 361 AU 0788 413 348
Mtalaamu wa Tiba Asilia ya Binadamu Top Manyota. Fika Uwanja wa Nyamagana ili kuonana nae live.
Mwanza Wine pia wapo. Kwa wale wanaojua kuitendea haki kiu yao ya kinywaji basi hapa ni mahali sahihi wawapo katika maonyesho ya Biashara ya Afrika Masharika yanayoendelea katika Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Hapa ni Mambo ya Viatu tena kwa bei nafuu.
Hapa Mambo ya Majiko ya Gesi ndo mahala pake. Oryx wanawakilisha kama kawaida ndani ya Nyamagana.Pia kuna ofa kwa ajili yako.
"Wahi Ofa yako kabla Maonyesho hayajaisha"
"Bring Bring ni Hapa. Njoo upendeze kwa bei nafuu"
Ukiingia Nyamagana kama umeambatana na Mmeo/ Mpenzi au Mchumba hakikisha unafika katika banda la TRESSA ili upendeze.
Balozi wa China nchini Tanzania Li Xuhang (katikati) akikagua mabanda.
Taswira ya Uwanja wa Nyamagana jinsi ilivyo.
Na Jacktan Msafiri: Mtanzania Media

No comments:

Powered by Blogger.