LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAASISI YA ANGELS MOMENT YATOA SOMO KWA WANAWAKE MKOANI MWANZA.


Taasisi ya Angels Moment ya Jijini Dar es Salaam jana imewakutanisha pamoja Jumla ya Wanawake Wajasiriamali 500 Mkoani Mwanza, kwa lengo la
kuwapatia elimu ya Msingi juu ya Masuala mbalimbali ya Ujasiriamali ili kuziba changamoto zinazowakabili katika Masuala ya Ujasiriamali.

Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto pamoja na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), imewakutanisha wanawake hao Wajasiriamali kupitia Kampeni yake ya Mwanamke na Uchumi ambayo imelenga kuwapatia wanawake elimu ya Ujasiriamali kulingana na fursa zilizopo katika mazingira yao, Kampeni ambayo imelenga kuwafikiwa wanawake wajasiriamali katika Mikoa mbalimbali hapa nchini.
Neema Malima ambae ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Angels Moment.
Kwa Mkoa wa Mwanza Kampeni hiyo ya Mwanamke na Uchumi imefanyika katika Uwanja wa Magomeni Ulioko Kirumba Wilani Ilemela na itadumu kwa siku mbili ambazo ni leo Alhamisi Septemba nne na Kesho Ijumaa Septemba tano ambapo hakuna Kiingilio.

Neema Malima ambae ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Angels Moment iliyoandaa Kampeni hiyo ya Mwanamke na Uchumi, amebainisha baadhi ya mafunzo yanayotolewa ni pamoja na ujasiriamali na fursa zinazomzunguka mwanamke kabla ya kuanzisha biashara pamoja na usimamizi binafsi wa fedha na uwekaji wa akiba.
Amina Masenza ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Mafunzo mengine ni pamoja na Afya bora kwa mwanamke na Uchumi imara ambapo wanawake wanapewa elimu katika kutatua changamoto za magonjwa ya wanawake ambayo ni kikwazo katika shughuli zao.

Kwa Mkoa wa Mwanza Kampeni hiyo ya Mwanamke na Uchumi imewajumuisha Wanawake wajasiriamali kutoka Wilaya za Magu, Ilemela na Nyamagana huku pia Mikoa ya Kigoma, Tanga, Ruvuma, Dodoma, Pwana na Lindi ikitarajiwa kunufaika na Kampeni hiyo hapa nchini.

Akizungmza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amina Masenza ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela amewataka wanawake waliohudhuria katika Kampeni hiyo kuwa chachu ya Maendeleo kwa kufanya biashara endelevu na yenye tija kwa kujiwekea akiba sanjari na kutumia faida faida ya biashara yao katika kujiongezea mtaji.

Amewasihi zaidi kutumia daftari katika kutunza taarifa zao kwa kuwa biashara bila daftari huisha bila taarifa huku pia akiwasihi akinamama hao waliohudhuria katika Kampeni hiyo ya Mwanamke na Uchumi Mkoani Mwanza kujenga tabia ya kupima afya mara kwa mara wao na familia zao kwa lengo la kutambua afya zao jambo litakalowasaidia wao na familia zao katika kumudu shughuli zao vyema.

Aidha ametoa wito kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza kuhakikisha kwamba Maafisa Maendeleo ya Jamii wanatumika ipasavyo katika kuwahudumia wananchi ambapo amewasihi akina mama kufika katika ofisi za Maafisa Maendeleo ya Jamii walio katika Halmashauri zao kwa lengo la kupata huduma kwa kuwa Maafisa Maendeleo hao wameajiriwa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.

Katika Kuhitimisha hotuba hiyo aliyoisoma kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Masenza ametoa tahadhari kwa akina mama kujiepusha na vitendo viovu ambavyo vimekuwa vikitendeka katika maeneo mbalimbali hususani kwa wavuvi ambapo wanawake wamekuwa wakitumika kingoko katika kujipatia mahitaji yao kupitia mfumo uitwao hamsini kwa hamsini ambapo mwanamke hulipia nusu ya gharama ya mahitaji yake na nusu nyingine inayobaki mwanamke huilipia kwa njia ya ngono.

Kwa Upande wake Paul Manyika ambae ni Afisa Viwango kutoka Shirika la Viwango nchini TBS amewashauri akina mama wajasiriamali kufuata taratibu zilizopangwa ambazo ni pamoja na kulipia gharama zilizoidhinishwa na TBS kwa ajili ya bidhaa zao kupata usajili, huku akiwasihi wale ambao hawana uwezo wa kulipia gharama hizo kuanzia katika Shirika la SIDO ambapo Serikali inawasaidia akina mama wajasiriamali bure ama kwa bei nafuu kupitia mfuko wa wajasiriamali badala ya kudhania kwamba TBS imewatenga hivyo haiwahudumii.

Kuhusiana na hali ya Ushindani wa Soko la Afrika Mashariki, Manyika amesema kuwa ushindani si mkubwa sana japo amewashauri wajasiriamali kulitumia Shirika la Viwango nchini TBS katika kuboresha bidhaa zao kwa kuwa shirika hilo pia hutoa elimu inayoweza kumfanya mzalishaji kutengeneza bidhaa bora zinazoweza kuuzika hadi nje ya nchi.

Nae Stella Mrosso ambae ni Mkuu wa Maabala ya Chakula TBS amebainisha kuwa asilimia kuwa ya sampuli wanazozipokea kwa ajili ya vipimo zinatoka kwa wajasiriamali wadogo ambao wanataka kujiinua na kupata ubora wa TBS.

Amesema changamoto kubwa iliyopo kutoka kwa wajasiriamali walio wengi ni kutofuata taratibu za uzalishaji ikiwa ni pamoja na kujishughulisha na uzalishaji katika maeneo ya nyumbani jambo ambalo haliruhusiwi hata katika sheria za uzalishaji kwa kuwa huathiri ubora wa bidhaa zinazozalishwa, na hivyi akawasihi wajasiriamali kuendelea kujifunza zaidi ili waweze kuzalisha bidhaa ambazo ni bora kulingana na viwango vya TBS.
Akina Mama Wajasiriamali waliohudhuria Kampeni ya Mwanamke na Uchumi katika Uwanja wa Magomeni Kirumba Mkoani Mwanza.
Altaf Mansoor ambae ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta MOIL. Akifurahia wakati Linah Alipokuwa akitoa Burudani.
Neema Malima ambae ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Angels Moment (Kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Bi.Amina Masenza (Kulia).
Bi.Sauda Shabani Kutoka Pwani (Kulia) akisoma Shairi la Kuwahamasisha akina mama katika Kampeni hiyo ya Mwanamke na Uchumi. Kushoto ni Afisa Mawasiliano Taasisi ya Angels Moment.
Msanii Linah Sanga ambae ni pia ni Balozi wa Kampeni ya Mwanamke na Uchumi akitoa burudani kwa Wamama Wajasiriamali wa Mkoa wa Mwanza.
Linah Akiimba Wimbo Maalimu kwa ajili ya Kampeni ya Mwanamke na Uchumi.Linah ni balozi wa Kampeni hiyo.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.