LIVE STREAM ADS

Header Ads

BANK YA MKOMBOZI YAKABIDHI MSAADA KWA WATOTO YATIMA WA KIJIJI CHA MATUMAINI MWANZA.

Meneja  wa benki  tawi la Mwanza bwana  Nichorus    Mokirya  akitoa  hotuba wakati wa kukabizi misaada  katika kitu  cha watoto  yatima  cha Kijiji  cha  Matumaini kilichopo  Nyegezi, Jijini mwanza.
Banki  ya Mkombozi  Tanzania   imeendelea kurudisha sehemu  ya  faida  yake  kwa kuwasaidia  watoto  yatima wanaolelewa  katika nyumba ya  kuwatunza  watoto  yatima  ya Kijiji cha Matumaini ilichopo Nyegezi, Wilaya  ya  Nyamagana  Mkoni Mwanza.

Akitoa hotuba fupi
jana katika hafla ya  kukabidhi  msaada wao  kwa Kijiji hicho, Meneja  wa  Mkombozi  tawi  la Mwanza  Bwana  Nichorus   Mokirya  kwa  niaba ya  mkurugenzi mtandaji wa  benki hiyo,  alisema kuwa  benki yake  imeendelea  na utaratibu wa  kutoa  sehemu  ya  faida  yake  kwa ajili ya kuisaidia  jamii  katika  Nyanga  ya  elimu  na kutoa  kipaumbele  kwa watoto wasio   na  wazazi  au walezi  yani  yatima.

Bwana   Mokirya   aliongeza kuwa  Taifa lolote  ili  liendeleaa  linahitaji   watu wake  kuwa  na elimu, hivyo basi  wao  kuwekeza  katika  elimu ni  maaamuzi  sahihi  kwao na  hawatajutia   uamiuzi  huo.

Aliwataja watoto watakaonufaika na msaada huo kuwa ni, Nacy  Osacar  mwanafunzi wa kidato  cha tatu, Kashuliza  Kamugisha mwanafunzi wa kidato  cha  pili na  Peter  Aklan  mwanafunzi wa kidato cha kwanza, ambao wote  wanasoma  katika  shule  ya  Sekondari Twihulumile.

Pia  bwana  Mokirya alitoa  rai  kwa  wadau  wengine  kuwa  na  desturi za  kuwasaidia    watoto  yatima  kwa kuwa hawana  walezi  na  wanaitegemea  jamii  inayowazunguka  kuweza  kuwasaidia.
Benki  ya  Mkombozi  imekuwa  itoa  huduma  mbalimbali za  kibenki  na  hivyo basi   faida  wanayoipata  wanagawa  sehemu  ya faida    hiyo  na kuirejesha  kwa jamii  kupitia  misaada  ya  kielimu.


Naye Katibu wa  Chama  Cha  Waandishi wa  Habari wa  Kupiga Vita Matumizi ya  Dawa za Kulevya   na  Uhalifu   Tanzania OJADACT, Dennis  Mpagaze  alisema  kuwa  huduma   zinazotolewa na benki  hiyo  ni  za kiwango  cha  juu  na kinachowavutia  watanzania  wengi  kupata  huduma  za kibenki  katika  benki hiyo,  hali iliyopelekea hata  chama  hicho  kufungua  akaunti  ya  chama  katika  benki hiyo.
Na:Edwin Soko.

No comments:

Powered by Blogger.