TAARIFA YA OJADACT KWA WANAHABARI KUHUSU WASANII KUJIHUSISHA NA DAWA ZA KULVYA NCHINI.
NDUGU WAANDISHI WA
HABARI, CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WANAOPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA
KULEVYA NA UHALIFU (OJADACT) KIMETOA TAARIFA
HII FUPI KWA VYOMBO VYA HABARI
BAADA YA WAANDISHI
WENGI
KUTAKA KUJUA NI “KWA NINI WASANII WAMEKUWA
WAKIJIHUSISHA ZAIDI NA TUHUMA ZA
KUSAFIRISHA NA KUTUMIA DAWA ZA KULEVUA”?.
OJADACT KWA MUDA
MREFU TUMEKUWA TUKIFUATILIA TATIZO HILI
NA HATIMAYE KUAMUA KUTOA
TAARIFA HII KWENU
BAADA YA KUFANYA
UCHUNGUZI ULIOANZA MWANZONI
MWA MWAKA 2014.
BAADA YA TUKIO
LA HIVI KARIBUNI
LA KUSHIKWA KWA BAADHI YA WASANII
NA DAWA ZA KULEVYA, TAASISI HII
IMEKUWA IKIPOKEA MASWALI MENGI HUU YA MATUKIO HAYO, HALI
ILIYOTUSUKUMA KUTOA UTAFITI WETU
KWA MUDA HUU KWENU ILI
KUWEZA KUINUSURU JAMII
NA JANGA LA DAWA ZA KULEVYA.
ZIFUATAZO NI SABABU
KUBWA ZA WASANII/WANAMICHEZO KUJITUMBUKIZA KWENYE BIASHARA
YA MATUMIZI NA USAFIRISHAJI WA
DAWA ZA KULEVYA:
•UMAARUFU WAO NA
MVUTO MBELE YA WAFANYABIASHARA WA DAWA ZA KULEVYA, UNAWASHAWISHI
KUWATUMIA WASANII KWA AHADI
ZA KUWALIPA MALIPO MAKUBWA ILI WAENDELEE KUWA MAARUFU NA KUWA NA MAISHA MAZURI.
Kwa kuwa wasanii ni watu maarufu na wenye
mvuto kwa jamii, mara nyingi wafanyabiashara wa
dawa za kulevya
wanashawishika nao kutumia
kundi hili ili kuweza
kufanikisha mambo yao yaende
na kuharibu maisha
ya wasanii hasa wanaposhikwa na kuharibu
ndoto zao.
•URAHISI WAO WA
KUPATA VIZA ILI KUINGIA NCHI ZA UGHAIBUNI KWA LENGO LA
KUFANYA MAONYESHO MBALIMBALI .
Wafanyabishara wa
dawa za kulevya wanatumia mwanya wa urahisi wa
kujenga hoja ya kusafiri
kama wasanii/ wanamichezo kupata
viza za kwenda kufanya
maonyesho Nchi za ughaibuni, kwani
kwa msanii ni rahisi
zaidi kupata viza hizo kuliko mtu wa kawaida ambaye ni
kazi kujenga ushawishi huo.
•KIPATO KIDOGO KWA
WASANII NA MAISHA
YA KIFAHARI.
Wauza dawa za
kulevya wamekuwa wakisoma alama za nyakati kwa kubaini
wengi wa wasanii wamekuwa na kipato kidogo, huku jamii ikiamini
wao ni mamilionea, hapo ndipo wafanyabiashara hao
wanapotumia mwanya wa kuwarubuni
baadhi yao kuingia katika biashara hiyo ili
waweze kuwa mamilionea na kuishi
maisha wanayofanana na majina yao.
•KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KAMA VICHANGAMSHI KATIKA MAONYESHO YAO
(STIMULANTS) (PSYCHOLOGICAL DEPENDENCE).
Wasanii wengi
wanatumia dawa za kulevya kama
vichangamshi katika maonesho mbalimbali kwa lengo la kuwavutia
wapenzi wao, hali hiyo inawafanya kuwa wategemezi wa dawa za kulevya na kuwafanya kila
wanaposafiri toka eneo moja
kwenda eneo jingine lazima
wahakikishe wana dawa za kulevya. Hapo
ndipo baadhi yao wanashikwa na dawa hizo wakiwa kwenye
vituo vya kusafiria (Viwanja vya ndege, bandari na mipaka
ya nchi kavu).
•UELEWA MDOGO
JUU YA DAWA ZA KULEVYA.
–Jamii likiwemo kundi
hili la wasanii halina uelewa na tatizo la dawa kulevya hasa
faida na hasara zake, kwani mwelekeo
umebaki kuwa mmoja tu yani
kutafuta uchangamfu(Stimulants),
vileta njozi/maruweruwe (Hallucinogens) na vipumbaza (Depressants) bila kujali
madhara yake ya kimwili, kiakili na kiroho sanjali
na utegemezi.
MAPENDEKEZO YETU:
•ELIMU KWA JAMII
NZIMA INAHITAJIKA KUJENGA
UELEWA WA DAWA ZA KULEVYA.
Ni vyema sasa
jamii wakiwemo wasanii wakapata
elimu tosha ya
dawa za kulevya kwa kujua hatari ya kujiingiza
kwenye matumizi ya dawa za kulevya na madhara
yake hasa katika utegemezi.
•IANZISHWE
KAMPENI MAALUMU KWA WASANII.
Kampeni hiyo itasaidia
wasanii kufundishwa umuhimu
wao katika Taifa katika
kulinda heshima na Nchi
na uwakilishi mwema katika Nyanja
za kimataifa.
•SERIKALI
ITAZAME NAMNA YA KUSIMAMIA
HAKI ZA WASANII.
Endapo kazi za wasanii
zitasimama vyema ni wazi kuwa
wasanii watapata maslahi mazuri
ya kazi zao na kuongeza
kipato chao badala
ya sasa kuibiwa kazi zao
na kubaki na umaskini
hatimaye kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.
NDUGU ZANGU WAANDISHI
UCHUNGUZI WETU NI MREFU
LAKINI TUMETUMIA KUONESHA SEHEMU
NDOGO TU INAYOSADIFU
TATIZO LA SASA
ILI KUWAPA HALI HALISI
KWA MANTIKI YA NINYI KUIELIMISHA
JAMII HII WAKIWEMO
WASANII WAJIEPUSHA NA BIASHARA
HII.
Imeandaliwa na
OJADACT na Kutolewa na;
Edwinn
Soko, Mwenyekiti 30/10/2014.
No comments: