MEYA WA JIJI LA MWANZA AWATAKA WANANCHI KUJIEPUSHA NA KAULI ZA WANASIASA AKIWEMO WENJE.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza
Stanslaus Mabula amewataka wananchi wa Kata ya
Pamba na Jiji la Mwanza kwa Ujumla kutodanganyika na maneno ya wanasiasa ambayo hayalengi kuchochea maendeleo
kwa wananchi.
Mabula ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani
Jijini Mwanza (CCM) alisema hayo
juzi wakati wa usimikaji wa kamanda mpya wa umoja
wa vijana( UVCCM) Kata ya Pamba Rordrick Ngoye
na kuongeza kuwa chama cha mapinduzi kitaendelea kupuuzwa kotokana na
watu wachache wanao kichafua kwa maslahi yao binafsi.
Alieleza kuwa vyama vya siasa vimekuwa
vikiwadanganya wananchi kuwa wao ndio wameleta maendeleo na kukipinga chama
kilichopo madarakani kwa madai kuwa hakileti maendeleo kwa wananchi wake.
Akimzungumzia Mbunge Jimbo la Nyamagana Ezekia Wenje (CHADEMA), Mabula
alieleza kuwa mbunge huyo amekuwa akijitapa kwamba Chama chake ndicho kimefanya
juhudi za ujenzi wa barabara za Karuta,
Butimba Mkuyuni na Kiloleni huku akidai
wafanyabiashara ndio waliongoza kulipa kodi za ujenzi wa daraja la
Mabatini, wakati ni jukumu la kila mfanyabiashara kulipia kodi hiyo.
“Kwa nini hakuthubutu kusema kuwa yeye
ndio ameweka daraja la mabatini? badala yake alisema anawashukuru wafanyakazi
kwa kulipa kodi na polisi kwa kuchangia kodi”alisema Mabula akinukuu kauli
aliyoitoa Wenje hivi karibuni Mkoani wakati Rais Kikwete alipofanya ziara
Mkoani Mwanza na hivyo kuwataka wananchi kujiepuka nae sanjari na kauli za namna hiyo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa CCM Wilaya
ya Nyamagana Raphael Shilatu aliwasisitiza zaidi wananchi kuipigia kura katiba
iliyopendekezwa pindi wakati wa kufanya hivyo utakapowadia ili kuweza kuleta
maendeleo kwa wananchi wote kwani Katiba inayopendekezwa imetoa haki kwa kila
mmoja.
Na:Prisca Japhes
SIASA BWANA ZINA RAHA YAKE...LAKININ KWENYE SIASA HAPA NCHINI WOTE NI WALE WALE TU.HAWANA JIPYA.WOTE WALAJI TU.
ReplyDelete