LIVE STREAM ADS

Header Ads

MADUDU YASABABISHA KIKAO CHA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA SERIKALI ZA MITAA KUAHIRISHWA JIJINI MWANZA.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa Rajab Mbaruku (katikati) akiahirisha Kikao cha Tathmini juu ya Shughuli za Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo zilizofanyika Mkoani Mwanza.Wa Kwanza Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo na Wa kwanza Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara Mkoani Mara ambae ni mmoja wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa.
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa imeshindwa kufanya Kikao chake cha Tathmini ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo katika Mkoa wa Mwanza, licha ya Kamati hiyo kubaini mapungufu mbalimbali katika Miradi ya Maendeleo iliyokaguliwa Mkoani Mwanza.

Kikao hicho kilipangwa kufanyika
hii leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, kiliahirishwa muda mfupi baada ya kufunguliwa kutokana na kukosekana kwa Mwakilishi kutoka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI licha ya Wizara hiyo kupewa taarifa ya kuhudhuria kikao hicho.

Akitoa hoja ya Kuahirishwa kwa kikao hicho, Mjumbe wa Kamati hiyo Mh.Kange Lugola alieleza kwamba Kamati hiyo imebaini ufisadi wa hali ya juu katika Miradi mbalimbali ya Maendelo Mkoani Mwanza, hivyo isingeweza kutoa tathmini yake kutokana na TAMISEMI kutohudhuria kikao hicho kwa kuwa baadhi ya watendaji kutoka Wizara hiyo nao wanahusika katika usimamizi wa miradi iliyoonekana kugubikwa na ufisadi huo.


Lugola aliitaja baadhi ya Miradi iliyogubikwa na Ufisadi Mkubwa katika Mkoa wa Mwanza kuwa ni pamoja na Uuzwaji wa Jengo la iliyokuwa Kliniki ya Akina Mama na Watoto Makongoro na Ujenzi wa Kliniki kama hiyo katika eneo la Mirongo katika Jiji la Mwanza pamoja na ubadhirifu wa fedha katika ujenzi Mradi wa Maji katika Halmashauri ya Mji wa Sengerema.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Ebarist Ndiki (Mwenye Kinasa Sauti).
Akizungumzia Uuzwaji wa Jengo la Kliniki ya Makongoro, Lugola amesema kuwa kamati imebaini kuwa jengo hilo lilipaswa kuuzwa shilingi bilioni Sita, lakini kutokana na janja janja ya Viongozi wakiwemo wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na TAMISEMI, jengo hilo liliuzwa kwa Bank kuu ya Tanzania shilingi bilioni tatu, huku Kliniki mpya ya Akina Mama na Watoto iliyojengwa Mirongo ikibadilishwa mchoro wake uliokuwa wa ghorofa na kujengwa jengo fupi ambalo haliendani na fedha zilizotengwa katika ujenzi wa Kliniki hiyo ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni Moja.

Kuhusu Mradi wa Maji katika Wilaya ya Sengerema ambao ulitengewa Shilingi Bilioni Moja na Milioni 400 kwa ajili ya kujenga miundo mbinu ya maji ya Ziwa Victoria kutoka eneo la Lumea kwenda katika Kijiji cha Nyehunge na Karebezo, Lugola alisema kuwa Kamati ilibaini kuwa Mradi huo badala ya kujengwa tenki lenye ujazo wa Lita Laki Moja, ulifanyika tu ukarabati wa tenki la Lita 90 lililojengwa enzi za ukoloni kwa kutumia gharama zilizotengwa.

Kutokana na hali hiyo, Lugola alitoa hoja ya kumuomba Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa kuahirisha Kikao chake cha Tathmini ya Miradi iliyokaguliwa na Kamati hiyo Mkoani Mwanza, hoja ambayo iliungwa Mkono na Mwenyeti wa Kamati hiyo Mh.Rajab Mbaruku.

Akiahirisha kikao hicho,Mbaruku alibainisha kwamba Kamati hiyo inatarajia kukutana Jijini Dar es salam kabla ya Kuanza kwa Vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vinavyotarajia kuanza Wiki ijayo ambapo suala la ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo Mkoani Mwanza litawasilishwa kwa ajili ya kujadiliwa zaidi.


Akizungumza kabla ya Kuahirishwa kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo ameishukuru Kamati hiyo kutokana na Kazi iliyoifanya Mkoani Mwanza, ambapo aliwataka Viongozi na Watendani Mkoani Mwanza kujitathmini katika Utendaji wao, badala ya kusubiri Kamati za Bunge katika kuibua ari ya utendaji kazi wao.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo (Kulia) akiwa na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge.
Viongozi na Watendaji mbalimbali Mkoani Mwanza.
Viongozi na Watendaji mbalimbali Mkoani Mwanza.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa (Wawili kulia) wakiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mtumushi wa Mungu Baraka Konisaga (Wa Tatu kulia).
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa (Wawili kushoto) wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Ebarist Ndikilo (Wa Kwanza Kulia).
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa.
Taswira katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ilivyokuwa katika Kikao cha Tathmini juu ya Shughuli za Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo zilizofanyika Mkoani Mwanza.
Taswira katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ilivyokuwa katika Kikao cha Tathmini juu ya Shughuli za Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo zilizofanyika Mkoani Mwanza.
Diwani wa Kata ya Kitangiri ambae pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Hennry Matata (Kulia) akisalimiana na watendaji mbalimbali kutokana Halmashauri ya Jiji la Mwanza baada ya Kuvunyika kwa Kikao cha Tathmini juu ya Shughuli za Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo zilizofanyika Mkoani Mwanza.
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa Mh.Kange Lugola (Kulia) ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara Mkoani Mara (CCM) akizungumza na Waandishi wa Wanahabari baada ya Kuvunyika kwa Kikao cha Tathmini juu ya Shughuli za Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo zilizofanyika Mkoani Mwanza.
MSIKILIZE HAPA CHINI KANGE LUGOLA:

Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.