LIVE STREAM ADS

Header Ads

DENDEGO: CHANGAMKIENI FURSA ZA MWANAMKE NA UCHUMI.

Mkuu wa wilaya ya Tanga mheshimiwa Halima Dendego (Kushoto) akitoa wito
kwa taasisi na mashirika mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi za
kampeni ya mwanamke na uchumi Zinazotolewa na kampuni ya Angels Moment
ili kumkomboa mwanamke mjasiriamali.
Wanawake Wajasiriamali Mkoani Tanga wametakiwa kujitokeza na kuchangamkia fursa zitakazotolewa na kampeni ya Mwanamke na Uchumi inayotarajiwa kutolewa mwanzoni mwa mwezi ujao Mkoani Tanga ambapo zaidi ya wanawake 300 watanufaika na mafunzo hayo yanayotolewa na kampuni ya Angels Moment ya jijini Dar Es Salaam.


Mkuu wa
Wilaya ya Tanga Mh.Halima Dendego amesema fursa zitakazotolewa ni fahari kwa wanawake na wajasiriamali wa mkoa huo kwani elimu inahitajika sana wakati huu wa ushindani wa biashara.

 “Fursa kama hizi mara nyingi ni nadra kuzipata na Kampeni ya mwanamke na uchumi ni jibu la changamoto mbalimbali kwa wajasiriamali kwani elimu watakayoitoa ni fursa pekee ya kusonga mbele kibiashara na kiuchumi kwa wanawake wa mkoa wa Tanga” alisema.

Mkuu huyo wa wilaya amewaomba  Wadau mbalimbali waendelee kujitokeza kuunga mkono juhudi za Kampeni ya mwanamke na uchumi kwani kupitia akina mama huduma zao zitaweza kufahamika na kunufaika kwani ndiyo nafasi pekee ya kukutana na wajasiriamali na kusaidia kuinua uchumi wa akinamama na Taifa kwa ujumla.
Mkurugenzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi Mahada Erick
(kulia) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kampeni
ya mwanamke na uchumi itakayotolewa tarehe 5 na 6 mwezi ujao mkoani
Tanga,kushoto ni mkuu wa wilaya ya Tanga mheshimiwa Halima Dendego.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi  Mahada Erick amesema kuwa  kampeni ya mwanamke na uchumi ni jawabu la changamoto zinazokumba biashara na ujasiriamali kwani elimu na semina zitakazotolewa zitawapa msingi wa kuanza upya kuandaa biashara na ujasiriamali kwa ujumla na pia kutoa hamasa kwa akinamama katika kujiletea maendeleo.


“ Kampeni hii inalenga kutoa hamasa na ari kwa akinamama kusonga mbele kimaendeleo, Hakuna ubishi kuwa akinamama wana juhudi kubwa sana za kutafuta fursa za kujiongezea kipato, ila tatizo ni elimu ya msingi ya kuangalia fursa zinazowazunguka na jinsi ya kuendeleza biashara zao.”

Angels Moment itawakutanisha akinamama waliofanikiwa kibiashara na ambao wanafanya ujasiriamali mbalimbali ili kuelezana mbinu mbalimbali za mafanikio. Pia kutakuwa na wataalamu watakaotoa elimu ya ujasiriamali, uwekezaji, uwekaji akiba na elimu ya afya’ anasisitiza.

Kampeni ya Mwanamke na uchumi Mkoani Tanga itafanyika tarehe tano na sita mwezi ujaokatika Ukumbi wa Naivera  ambapo utapambwa na msanii Linah Sanga ambaye ni balozi wa Wanawake.Wadau walioungamkono kampeni ya mwanamke na uchumi ni MKoani Tanga ni pamoja na SSRA,NSSF,TBS,PSPF,GEPF,AGHAKHAN HOSPITAL,MINJINGUMAZAO,HSC, na NAIVERA COMPLEX
Mkurugenzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi (Kulia) Mahada Erick
akijibu maswali ya Waandishi wa habari katika ukumbi wa naivera mjini
Tanga hivi karibuni katika maandalizi ya kampeni ya mwanamke na uchumi
itakayofanika hivi karibuni mkoani Tanga.
Mkurugenzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi Mahada Erick (Kushoto)
akisikiliza swali la mwandishi wa Gazeti la Daily news , Hayupo pichani
,katika ukumbi wa Naivera jijini Tanga ikiwa ni maandalizi ya kampeni
ya mwanamke na uchumi mkoani humo.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari
mkoani Tanga wakimsikiliza Mkurugenzi wa kampeni ya mwanamke na
uchumi,hayupo pichani juu ya kampeni ya mwanamke na uchumi inayoanza
hivi karibuni mkoani Tanga.
Na:Christian Gideon, Angels moment.

No comments:

Powered by Blogger.