LIVE STREAM ADS

Header Ads

SERIKALI YATAKIWA KUWALINDA WALEMAVU WA NGOZI HAPA NCHINI.

Serikali imetakiwa kuendelea kuwalinda walemavu wa ngozi nchini (Albino), hususani wale wanaoishi vijijini.

Akizungumza wikendi hii
ofisini kwake, Katibu wa walemavu wa ngozi (Tanzania Albino society) Mkoani Mwanza Mashaka Enos, alieleza kuwa albino waishio vijijini hawana amani na huofia kuuwawa muda wowote kutokana  ulinzi wao kuwa mdogo.

Pamoja na kuhitaji msaada kutoka serikalini, amewataka wananchi waishio vijijini kuimairisha ulinzi katika maeneo yao pamoja na kuwalinda walemavu wa ngozi waishio vijijini kwani wao wanaitaji uangalizi wa makini  na kwamba vijijini  ndio waathiriwa zaidi ukilingaanisha na mijini.

“ Vijijini hakuna ulinzi wa kutosha ndio maana mauaji ya Albino yako vijijini, pia makazi ya watu huchangia kwa kuwa mbali baina ya kaya moja na nyingine tofauti na ilivyo sehemu za mijini” alisema Enos.

Hata hivyo alitoa wito kwa jamii kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha mauaji ya Albino yanakomeshwa nchini, hususani mikoa ya kanda ya ziwa kwa lengo la kuendelea kulinda amani na utulivu wa Nchi.

“Kama mauaji ya walemavu wa ngozi bado yanaendelea, mtu utawezaje kusema nchi yetu ina amani na utulivu wakati sisi Albino tunaishi kwa kujificha kwa kuhofia maisha yetu? alihoji Enos.
Na:Prisca Mshumbuzi.

No comments:

Powered by Blogger.