UFISADI WA ESCROW UNAUNGWA MKONO NA VIONGOZI WA SERIKALI.
Baadhi
ya viongozi wa kisiasa nchini wamesema
sakata la akaunti ya
ESCROW linaungwa mkono
na baadhi ya viongozi wa Serikali wasio waaminifu wanaojilimbikizia mali
huku wakiliacha Taifa
likiwa maskini na wachache
wakijilimbikizia mali.
Hayo
yalibainishwa hivi karibuni Mkoani Mwanza na Mbunge wa
Kigoma Kusini
kupitia NCCR Mageuzi
David Kafulila na
Dokta Hamis Kigwagala, wakati wa
mdahalo wa wazi ulioandaliwa
na Chama Cha
Waandishi wa Habari za Kupiga
Vita Matumizi ya Dawa za Kukevya na
Uhalifu Tanzania (OJADACT).
Kwa
upande wake kafulila alisema
kuwa sakata la
akaunti ya ESCRO ni
ufisadi mkubwa unaofumbiwa
macho na baadhi
ya viongozi wenye
kunufaika na fedha hizo, huku wachache walio na uzalendo na
Nchi wakionwa ni wasaliti
kwa kuwa hawapo
tayari kuingia kwenye ufisadi
huo.
Kafulila alieleza
hayo mbele wa
washiriki wa mdahalo na
kuongeza kuwa sakata hilo
ni ufisadi mkubwa
ambao unaligharimu Taifa, kwani
takribani fedha Billioni mia
nne zimenyakuliwa na wajanja wachache, ambapo kimsingi
zingiweza kusaidia katika
kuboresha maisha ya watanzania.
Aidha Kafulila aliongeza kuwa
serikali isipowasilisha ripoti
ya uchunguzi wa sakata
hilo katika bunge
lijalo, basi yeye ataanzisha kampeni wa kuhamasisha wananchi kudai fedha
zao kwa kauli
mbiu ya “ Bring
Back our Money” yani
rudisheni fedha zetu.
Naye Mbunge wa Nzega Hamis
Kigwangala alisema kuwa, wapo wabunge
wachache ndani ya bunge ambao wanaamini kuwa watendaji wa wizara
ya nishati na madini wao ni miungu
watu ambao hawawezi kufanya makosa, matokeo yake ni
kulindwa kwa ufisadi
kupitia mikataba yenye
utata ndani ya wizara hiyo.
Kigwangala aliongeza kuwa CCM sio chama
kibaya bali baadhi ya viongozi
wake ndio wabaya, kwani
wamekuwa wakikiuka ilani ya chama
hicho kwa lengo la kujilimbikizia mali na kuwaacha watanzania
wakiwa maskini.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za
Kulevya na Uhalifu
Tanzania Edwin Soko, alisema kuwa
waliandaa mdahalo huo ili kuwapa nafasi wananchi kusikiliza nafasi ya bunge katika kulinda rasilimali za Taifa toka kwa baadhi
ya wabunge wa bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Soko
aliongeza kuwa OJADACT
wanapinga uhalifu wa ukiukwaji wa
katiba ya nchi na sheria zilizopo
unaofanywa na baadhi ya watendaji pamoja na wanasiasa wacheche kwa lengo la kujinufaisha
wao wenyewe.
Na Mwandishi wetu-Mtanzaniamedia Blog.
No comments: