LIVE STREAM ADS

Header Ads

REDIO 5 WAWAKUTANISHA WANASALAMU KUTOKA MIKOA ZAIDI YA 21,WAFANYA ZIARA KUWAONA WAGONJWA MT.MERU.

Baadhi ya Wanasalamu wa kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu njiro jijini Arusha wakikabidhi sehemu ya msaada wao kwa uongozi wa hospitali ya Mkoa Mt.meru juzi,kulia ni mratibu wa salamu kupitia kipindi cha usiku wa moto Yacob Simba kushoto ni Sista Shubi Mjawizi,anayefatia ni Sista Merry Stalla.
Yacob Simba akiongea na baadhi ya wanasalamu katika viwanja vya hospitali ya Mt.Meru anayefatia ni Godfrey Thomas ambao ni waratibu wa shughuli hiyo kupitia kituo cha Redio 5 katika kipindi usiku wa moto kinachorushwa kwanzia saa saba usiku hadi kumi na moja alfajiri kwa wiki nzima.
Yacob Simba akikabidhi ndoo ya mafuta  kwa uongozi wa hospitali ya Mt.Meru jana baadaa ya wanasalamu kutoka mikoa zaidi 21 kufika hospitalini hapo kuwafariji wagonjwa.
Vicky Mwakoyo ambaye ni Creative Meneja wa kampuni ya  Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha,katikati ni Yacob Simba  na Godfrey Thomas wakiwa wanajadili jambo.
Kulia ni Lucy Bongole ambaye ni mwanasalamu wakiwa wanajadiliana na wenzake katika viwanja vya hospitali ya Mt.Meru katikati ni Zuhura Mbise maarufu kwa jina la mama Sosy,kushoto ni Sister Monduly.
Wanasalamu wakiwa wanajadiliana.
Sehemu ya msaada uliotolewa na wanasalamu kwa wagonjwa hospitali ya Mt.Meru jijini Arusha.
Kushoto Mtangazaji maarufu wa Redio 5 kupitia kipindi chake cha  love cuts kinachorushwa jumatatu hadi ijumaa saa nne  hadi saa saba usiku Semio Sonyo  akiwa na mtangazaji machachari aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia kipindi chake cha usiku wa Moto kinachorushwa kwanzia saa saba usiku hadi kumi na moja alfajiri kwa wiki nzima  Godfrey Thomas aka GT wakifurahia jambo.
Nesi wa hospitali ya Mt.Meru Sista Merry Stella akitoa neno la shukrani kwa wanasalamu waliofika kuwatembela wagonjwa hospitalini hapo ambapo amewataka watu na mashirika mbalimbali kuiga mfano huo kwa kuwa mahitaji ya wagonjwa ni makubwa.
Muonekano katika hospitali ya Mt.Meru jijini Arusha.
Wanasalamu wakiwa wamevalia T-sheti za Redio 5.
Wapili kulia ni mmiliki wa jamiiblog Pamela Mollel wakwanza kushoto ni Godfrey Thomas aka GT wakiwa katika picha na baadhi ya wanasalamu jana zoezi hilo liliratibiwa na kituo cha Redio 5 kupitia kipindi cha usiku wa moto.
Baadhi ya wanasalamu wakisubiria kuingia katika wodi mbalimbali kuwajulia hali wagonjwa hospitalini hapo.
"Pole mama Mungu atakuponya"hayo ni maneno ya wanasalamu.
Yacob Simba mtangazaji wa Redio 5 akiwa anamjulia hali mama mgonjwa katika wodi ya wanawake.
Mwanasalamu mkongwe kutoka Arusha Baba Ali Mbondei(aliyevalia tisheti ya Redio 5)akiwa na wanasalamu wenzake wakimjulia hali mgonjwa katika wodi ya wanaume.
Wanasalamu wakiwa wanasoma dua kwa mgonjwa wodi ya wanaume katika hospitali ya Mt.Meru jijini Arusha.
Wanasalamu wakiwa wanaingia wodi ya saba kuwaona wagonjwa.
Godfrey Thomas  aka GT katikati akiwa amepozi na mashabiki wake ambao ni wanasalamu kupitia kipindi cha usiku wa moto cha kituo cha Redio 5 jijini Arusha.
Wanasalamu kutoka mikoa mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja vya hospitali ya Mt.Meru mara baada ya kufanya ziara ya kuwatembelea wagonjwa.
Habari Picha na Pamela wa Jamiiblog.

No comments:

Powered by Blogger.