LIVE STREAM ADS

Header Ads

KILIMO KINALIPA.NIMEFURAHISHWA SANA NA HII HALI WILAYANI TARIME.

Hawa ni Miongoni mwa Wakulima wanaopatikana katika Kitongoji cha Chira, Kijiji cha Kenyamanyori, Wilaya ya Tarime Mkoani Mara. Huku ndiko nilikozaliwa (George Binagi-GB Pazzo Managing Director wa Mtanzaniamedia Blog na Mtangazaji/ Mwandishi Metro Fm, Mwanza). Hivyo nikiwa Wilayani Tarime nilipata fursa ya kutembelea baadhi ya Mashamba ya wanafamilia wa Binagi (Kama wanavyoonekana katika picha).Hakika nilifarijika sana na kulingana na mazungumzo yao, Na nilibaini kuwa Kilimo Kinalipa na kinaweza kuleta mapinduzi makubwa nchini Tanzania.
Mahindi ni moja ya Zao ambalo linalimwa sana Wilayani Tarime kama zao la chakula na biashara.Jambo nililobaini hapa ni kwamba, wananchi hawa wakipwewa mbinu bora za kilimo wanaweza kupata tija zaidi kutokana na kilimo kwa kuwa wengi wa wakulima hawa wanalima bila kuzingatia kilimo cha kisasa, lakini jambo la kustaajabu ni kwamba mazao hupatikana, nivyo nikawaza na kubaini kwamba, kilimo cha kisasa kikitumika, mazao yatapatikana mara mbili au tatu zaidi.
Nilifurahishwa sana na Akina Mama hawa ambao nilikuwata wakiwa shambani wakichapa kazi ipasavyo.Hakika akina mama nao wanaweza wakiamua kwa sababu hawa wameweza hata kabla ya kuwezeshwa.
Hili ni Shamba la Mahindi la Mmoja wa Akina Mama hawa ambapo kwa umoja wao, huwa wanafanya zamu ya kwenda shambani kwa ajili ya palizi kulingana na Umoja wao huu.
Ardhi inayopatikana Wilayani Tarime hakika haibagui, mbali ya zao la Mahindi pia mazao kama Matikiti Maji pia hulimwa na kustawi vyema.Huyu ni mmoja wa wakulima wa siku nyingi kutoka Kitongoji cha Chira, Kijiji cha Kenyamanyori Wilayani Tarime ambae anafahamika kwa jina la Zakaria Isanchu.Anasema kwake yeye Kilimo ni kila kitu na amekuwa akilima mazao mbalimbali ikiwemo Mahindi, Mtama, Mhogo, Tikiti Maji, mazao ya mboga mboga, Matango, nyanya na mengine mengi kulingana na Neema ya ardhi inayopatikana Wilayani Tarime ambayo hukubali mazao mbalimbali.
Zao la Mhogo ni miongoni mwa mazao yanayolimwa kwa wingi Wilayani Tarime.Lakini kutokana mlipuko wa magonjwa katika zao hili, wakulima wengi wamebaki njia panda kwa kuwa zao hili kwa siku za hivi karibuni limeanza kushambuliwa sana na magonjwa hali ambayo imewafanya wakulima Kutoka Wilayani Tarime kupaza sauti zao ili watalaamu wa kilimo wawafikie na kuwapa ushauri juu ya namna ya kupambana na wadudu wanaoshambulia zao hili la mhogo.Picha imechukuliwa katika moja ya Shamba la mihogo lililopo Kitongoji cha Chira, Kijiji cha Kenyamanyori Wilayani Tarime.
Zao la Mahindi baada ya Palizi.Kwa sasa Wilayani Tarime wakulima wako katika msimu wa Palizi.
Zao la Migomba pia linalimwa sana Wilayani Tarime na hustawi sana.Hili ni shamba linalopatikana kwa wanaukoo wangu wa Binagi katika Kitongoji cha Chira, Kijiji cha Kenyamanyori Wilayani Tarime.Katika shamba hili pia mazao ya maharage yamelimwa kwa kuwa husaidia kulifanya shamba kuwa safi bila magugu.
Tofauti na Miaka ya zamani katika Kitongoji hiki cha Chira ambapo kulikuwa kunapatikana makundi makubwa ya Mifugo aina ya ng'ombe, kwa sasa wananchi wa kijiji hiki wanafuga ng'ombe wachache sana kwa ajili ya kilimo tu.
Hatimae Kamera ya Mtanzaniamedia Blog ikakutana na huyu bwana majira ya saa tano hivi akiwa anautendea haki mwili wake.Unaweza kudhani huo ugali unaliwa na watu 10, la hasha.Huo ugali unaliwa na mtu mmoja kama unavyomuona.Nilichobaini hapa ni kwamba, bado kitoweo cha nyama kina nafasi kubwa kwa wanatarime, lakini ule ugali wa mhogo na mtama wenyewe kasi yake imepungua tofauti na zamani.Sasa hivi wakurya wa Tarime wanakula ugali wa Mahindi tofauti na zamani ambapo zao la mahindi lilikuwa kwa ajili ya biashara, huku zao la mhogo na mtama likiwa ndo zao kuu la chakula katika familia.
Ze mimi George Binagi-GB Pazzo (Kushoto) @Radio Metro & Mtanzaniamedia Blog nikiwa na Shangazi yangu baada ya kumtembelea nyumbani kwake Kitongoji cha Chira, Kijiji cha Kenyamanyori Wilayani Tarime.Hakika nilifurahia sana uwepo wa Shangazi yangu.Vya kale ni dhahabu.Ahsante Shangazi yangu kwa Wosia wako.Mungu akuangazia Neema katika kipindi hiki cha uzee wako.
Na:George Binagi.

No comments:

Powered by Blogger.