LIVE STREAM ADS

Header Ads

MLETE MWANAO MAMIZI GRAND RESORT JIJINI MWANZA LEO.

Watoto wakiwa katika Maeneo yao ya kujidai ndani ya Kiwanja cha Mamiz Grand Resort kilichopo Mkolani-Malimbe Jijini Mwanza.
Wengi wa Wakazi na Jiji la  Mwanza sanjari na Wageni wanaofika Jijini Mwanza watakuwa tayari wamekwisha shuhudia mapinduzi ya Burudani kwa wote (Watoto na Watu Wazima) yanayopatikana Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani-Malimbe Jijini Mwanza.

Na kwa wale
wachache ambao bado hawajafika, basi bado hawajachelewa kwa kuwa Mamiz Grand Resort imeandaliwa mahususi kwa ajili ya watu wote ndani na nje ya nchi, ikiwa ni sehemu pekee ambayo inavutia kwa michezo ya watoto, vinywaji vya kila aina, vyakula mbalimbali sanjari na kila aina ya burudani.

Kumbuka Mamiz Grand Resort inapatikana kilomita chache tu kutoka katikati ya Jiji la Mwanza eneo la Mkolani  Centre-Malimbe ikiwa ni hatua chache pia kutoka Stand ya Mabasi Nyegezi.Ni sehemu pekee ambayo michezo mbalimbali ya Watoto inapatikana kila siku za wikendi huku huduma nyinginezo zikipatikana siku zote za juma.Pia ukiwa Mamiz Grand Resort na ukajihisi uchovu basi utakutana na vyumba safi na vya kiafrika huku vikiwa vimeandaliwa katika mazingira ya kitalaamu kabisa.
TAZAMA PICHA AMBAZO CAMERA YA MTANZANIAMEDIA BLOG ILIZINASA ILIPOTEMBELEA MAMIZI GRAND RESORT.
Hapa watoto wakagoma kabisa, wakasema wanahitaji kuweka kumbukumbu na George Binagi-GB Pazzo @Mtanzaniamedia Blog & Metro Fm.
Kumbukumbu baina ya Watoto na Managing Director wa Mtanzaniamedia Blog zikiendelea.
Kumbuku kama kawa na Watoto ndani ya Mamiz Grand Resort.


Hizi ni moja ya Nyumba za kulala ambazo zinapatikana ndani ya Mamiz Grand Resort.Kushoto ni General Manager wa Mamiz Grand Resort akiwa na Natty E kutoka Radio Metro.
General Meanager (Me) wa Mamiz akiendelea kutuonyesha mandhari ya Vyumba vinavyopatikana Mamiz Grand Resort.Pembeni ni Natty E kutoka Metro Fm.
Nyumba safi na za Kiafrika huku zikiwa zimenakshiwa kitalaamu kabisa ambazo zinapatikana Mamiz Grand Resort.
Na:George Binagi

No comments:

Powered by Blogger.