Washiriki wa Mkutano wa Viongozi wa Afya kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi Dr.Neema Rusibamayila ambae ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (Wa pili kutoka Kushoto waliokaa). Viongozi hao wamekutana hii leo Mkoani Mwanza kwa ajili ya Semna ya Siku mbili kuhusiana na Mradi wa Tibu Homa ambao unatekelezwa katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ukiwa na lengo la Kupunguza Maradhi na Vifo kwa Watoto walio chini ya umri wa Miaka Mitano kutokana na Magonjwa yanayosababisha Homa Kali kwa kuboresha ugunduzi wake na kutoa matibabu sahihi ya Magonjwa hayo.
Mshirika Mkuu wa Mradi wa Tibu Homa
ni Shirika la University
Research Co.,LLC (URC) kwa kushirikiana na Mshirika Mkuu Kitaifa ambae ni
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na wadau wengine ambao ni Shirika la
Amref for Health Africa, Management Science for Health (MSH) chini ya Ufadhili
wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID) ambapo Mradi huo
unatekelezwa katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Kagera, Mara,
Shinyanga, Simiyu na Geita. |
No comments: