LIVE STREAM ADS

Header Ads

BONANZA LA UFUNGUZI WA WIKI YA MLIPA KODI YA TRA LAFANYIKA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Mgeni rasmi kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi ambaye ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki akitoa nasaha zake kwa washiriki wa Bonanza hilo lililofanyika leo Novemba 15,2014 kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.Picha zote na Othman Michuzi.
Kaimu Mkurugeni wa Elimu na Huduma wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Allan Kiulla (kulia) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi lililofanyika leo kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.Bonanza hilo lililogeshwa kufanyika michezo mbali mbali,ikiwepo mpira wa miguu,mpira wa pete,kuvuta kamba na mingine mingi.Wa pili kulia ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki ambaye ndie alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Bonanza hilo.

Sehemu ya Wafanyakazi wa  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wafanyakazi wa NSSF ambao ni Waalikwa walioshiriki kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi wakifatilia kwa makini nasaha za Mgeni Rasmi,ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti".
Mtanange wa kukata na shoka kati ya Timu ya TRA na timu ya NSSF ulipigwa katika Uwanja wa TCC Chang'ombe,Mtanange uliowatoa kifua Mbele vijana wa NSSF kwa Mabao 4-2 dhidi ya wenzao wa TRA.
Mbio za kuku kwa kina Baba zilikuwa ni sehemu ya michezo iliyofanyika leo Uwanjani hapo.

Vijana wa Kundi la Wanne Star wakionyesha makeke yao mbele ya wadau wa TRA waliofurika kwa wingi kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo.
Na:Michuzi Blog.

No comments:

Powered by Blogger.