DIAMOND ASEMA ANATAMANI KUFANYA KAZI NA HUYU MSANII.
Tumeshasikia kuwa kuna msanii wa
Marekani ambaye Diamond Platnumz tayari amefanya naye collabo ingawa bado
hajamuweka wazi, lakini hivi karibuni alimtaja msanii mkubwa wa
Mareknai ambaye
ana ndoto ya kufanya naye pia collabo.
Akizungumza na show ya Sporah, Diamond
amesema licha ya kufanikiwa kufanya collabo na baadhi ya wasanii wakubwa wa
Africa kama Davido, Iyanya, Mafikizolo na wengine, lakini ndoto yake ya miaka
mingi ni kufanya wimbo na hit maker wa ‘Good Kisser’, Usher Raymond.
“Natamani nifanye wimbo na Usher
Raymond sana, natamani nifanye naye nyimbo kwasababu ni mtu ambaye nilikuwa
nikimtazama tangia mdogo nakua, nikifanya nae nahisi nitatimiza moja ya ndoto
zangu.” alisema.
Na:Bongo5
No comments: