LIVE STREAM ADS

Header Ads

OJADACT YAKUTANA NA WANAHABARI BAADA YA TUKIO LA KUTEKWA KWA MLEMAVU WA NGOZI MKOANI MWANZA.

NDUGU WAANDISHI WA HABARI CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WA KUPIGA  VITA  MATUMIZI  YA  DAWA ZA KULEVYA NA UHALIFU  TANZANIA (OJADACT) TUMEWAITA  HAPA KUZUNGUMZIA  UKATILI  ULIOFANYWA NA WATU  WASIOJULIKANA    DHIDI  YA   MTOTO  MLEMAVU WA NGOZI  PENDO  EMMANUEL (4) AMBAYE 
KIMSINGI  HADI  LEO  HAJAPATIKANA.

NDUGU WAAANDISHI WA  HABARI, CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WANAOPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA NA UHALIFU TANZANIA (OJADACT),  TUMESIKITISHWA  SANA NA TUKIO  HILI NA TUNALAANI  VITENDO  HIZI  KWANI  NI VYA  KIALIFU  NA VINAKWENDA  KINYUME  NA  KATIBA  YA  JAMHURI  YA MUUNGANO WA TANZANIA  IBARA  YA  14 INAYOSEMA KUWA “ KILA MTU ANA HAKI  YA  KUISHI  NA KULINDWA   MAISHA  YAKE  NA JAMII KWA MUJIBU WA SHERIA  ZA NCHI”

OJADACT   TUMEPATA  MAPENDEKEZO  (8)  AMBAYO  TUNAIMANI YATASAIDIA  KUKOMESHA   VITENDO  HIVYO  VYA KIKATILI, MAPENDEKEZO  HAYA  YAMETOKANA NA MAONI  YA  WANANCHI    ZAIDI YA  200  JUU  YA NINI  KIFANYIKE   ILI  KUMALIZA  TATIZO  LA MAUAJI  YA WALEMAVU  NCHINI.

TUMEFANYA  HIVI KWA KUWA  TUNAAMINI  KUWA ENDAPO  JAMII  IKIHUSISHWA  NA KUSIKILIZWA  ITASAIDIA  ZAIDI  KUJUA  WAHALIFU  WA VITENDO  HIVYO  NA HATA  NJIA SAHIHI YA  KUMALIZA  TATIZO  HILO, KWANI WAHALIFU HAO NI SEHEMU YA  JAMII.

MAPENDEKEZO
1:         SERIKALI  IUNDWE KIKOSI  KAZI CHA TAIFA CHA KUDUMU ILI KUWALINDA  WALEMAVU WA NGOZI.  TATIZO  HILI  NCHINI  LIMEKUWA NI KUBWA KIASI  CHA  KUHITAJI  NGUVU  MAALUMU  YA  KUTHIBITI  MWENENDO  HUU KAMA  TULIVYOKUWA NA  KIKOSI   KAZI CHA KUPAMBANA  NA  DAWA ZA KULEVYA    CHINI  YA KAMANDA  GODFREY NZOWA

2:         VIONGOZI  WA DINI  WATUMIKE ZAIDI  KATIKA KUTOA  MAUBILI YENYE  KUELIMISHA  JAMII  JUU  YA  ATHARI ZA   IMANI  POTOFU  ZINAZOENDELEA  KATIKA  USHIRIKINA KIASI CHA KUAMINI VIUNGO  VYA  WALEMAVU WA NGOZI  VINASAIDIA  MTU  KUPATA UTAJIRI,  TUNA IMANI  KWAMBA  VIONGOZI WA DINI WAPO HADI  VIJIJINI

3:         IUNDWE  TUME  MAALUMU  ITAKAYOWALAZIMU   WENYEVITI WA MITAA  NA VIJIJI  KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA  ULINZI WA  WALEMAVU WA  NGOZI   KWA KUHAKIKISHA  USALAMA WAO, KUWACHUNGUZA  NA KUWABAINI WAFANYABIASHARA  WA VIUNGO  VYA   WALEMAVU.

4:         SERIKALI  NA  ASASI  ZISIZO  ZA KISERIKALI  ZITUMIKE  KIKAMILIFU   KATIKA  KUTOA  ELIMU  JUU YA  MILA  POTOFU  JUU YA MAHITAJI  YA VIUNGO  VYA  WALEMAVU   KATIKA  KUPATA  UTAJIRI.

5:         VYOMBO  VYA  HABARI  VIWE  NA AJENDA  MAHUSUSI  YA KULAANI MAUAJI YA  WALEMAVU WA NGOZI  SANJALI  NA KUTOA  ELIMU  JUU  DHANA  POTOFU  YA  KUPATA UTAJIRI KWA KUUA.

6:         JAMII  KWA PAMOJA HASA  WAZEE WA KIMILA WAHUSISHWE  KWENYE  VIKAO  VYA KUTAFAKARI CHANZO  CHA  MAUAJI HAYO, KWANI  NI VYEMA  SASA JAMII  IKASHIRIKI  KIKALIFU  KUTAFAKARI JUU  YA MAUAJI  HAYO.

7:         SHERIA  ZILIZOPO  DHIDI  YA  WATU  WANAOJIHUSISHA  NA  MAUAJI YA  WALEMAVU WA NGOZI  ZISIMAMIE  ZAIDI  HAKI    BILA  KUHUSISHWA  NA  SUALA LA  RUSHWA  ILI KUPINDISHA  UTEKELEZWAJI WA SHERIA.

8:         MAMLAKA  NYINGINE  ZA KIUSALAMA  ZIUNGANE KATIKA  KUFUATILIA  CHANZO CHA   MAUAJI  YA  YANAYOENDELEA  KWA NDUGU ZETU WENYE  ULEMAVU WA NGOZI  KWA MUJIBU  WA SHERIA  ZA USALAMA WA NCHI

USHAURI  KWA WAZIRI WA MAMBO  YA  NDANI
OJADACT  TUNAMTAKA  WAZIRI  WA MAMBO  YA  NDANI  YA NCHI  MATHIAS  CHIKAWE  AFUPISHE MUDA WA  WIKI MBILI(2) ALIOUTANGAZA   WA KUANZA  KAZI  KWA KIKOSI  KAZI  ALICHOKITEUA KUFUATILIA MAUAJI YA ALBINO KATIKA  MIKOA 5  YA  MWANZA, SHINYANGA, SIMIYU, TABORA NA GEITA, KWANI  SUALA  LA  UHAI WA MTU  HALIHITAJI  SUBIRA  KAMA YA KWENDA  KUTOA POSA  KWANI  UHAI  HAUNUNULIWI MAHALI  POPOTE  PALE
RAI:
OJADACT  TUNAIOMBA JAMII, VYOMBO VYA  DOLA NA TAASISI NYINGINE  ZOTE    ZISHIRIKI KULAANI TUKIO  HILI   NA  KUTOA  TAARIFA  ZITAKAZOSAIDIA  KUPATIKANA  MTOTO  PENDO  KWA  VYOMBO  VYA DOLA, KWANI JAMBO HILI   LINAMGUSA  KILA  MMOJA WETU  NA  SI  VYEMA   KULIACHA  KWA  TAASISI  MOJA  TU YA  JESHI LA POLISI, KUSHIRIKI  KWA JAMII  NZIMA KUTASAIDIA  MAMLAKA ZA KIDOLA  KUFANYA  KAZI  ZAKE KWA  UFASAHA, NI  UKWELI USIOFICHIKA KUWA  WALIOJIHUSISHA NA KUFANKISHA  KUTEKWA  KWA MTOTO PENDO  NI  SEHEMU YA JAMII   TUNAYOISHI  NAYO, KWANI  VITENDO   HIZI NI  UKATILI MKUBWA NA VINALILETEA  TAIFA  SIFA  MBAYA  KATIKA MEDANI YA KIMATAIFA

             NAWASHUKURU SANA  NDUGU  WAANDISHI WA HABARI.
 EDWIN  SOKO

MWENYEKITI OJADACT.
16.01.2015.

No comments:

Powered by Blogger.