LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIONGOZI WETU MNAFANYA HAYA KWA MOYO WA DHATI AU KWA SHINIKIZO LA KAMERA?

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupanda Mgomba katika shamba la Kikundi cha Ushirika wa Tuko Imara unaojishughulisha na Kilimo cha Migomba na Mbogamboga  katika Kijiji cha Banda Maji,Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar siku ya Jana.

Kwa Mara kadhaa tumekuwa tukishuhudia viongozi mbalimbali wa Vyama vya Siasa na hata Serikali hapa nchini wakishiriki katika Shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na Ujenzi na hata Kilimo pindi wanapokuwa katika ziara zao.

Swali langu (Mwandishi) ambalo bado sijapata Mhusika hata mmoja wa kulijibu ni kwamba, ni kweli kile ambacho huwa tunakiona kutoka kwa viongozi hao huwa kinafanyika kwa mapenzi ya dhati au huwa ni kutokana na uwepo kamera hivyo wanaamua kutupiga changa la macho?

Pengine Swali hili laweza kuwa na majibu mengi kwani kila mmoja anaweza kuwa na jibu lake hivyo kupata jibu la mtu mmoja pia linaweza lisitosheleze mahitaji kwamba kinachofanywa na viongozi hao ni kwa mapenzi ya dhati ama la.

Mwisho wakati ukitafakari hayo, pia hoja yangu ya Msingi ni kwamba; Je kile kinachofanywa na viongozi hao huwa kinaashiria maisha yao halisi? Kama ameshiriki katika Shughuli za Kilimo basi anakijua kilimo na yuko tayari kukitumikia kilimo, kama ameshiriki shughuli za Ufugaji anaujua ufugaji na kuwa tayari kuutumikia Ufugaji nk.
TAZAMA PICHA KISHA NJOO NA MAJIBU YAKO.
Katibu mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kazi ya ujenzi wa barabara katika kijiji cha Kijini kwa Shauripili,jimbo la Shaani,wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar inayojengwa kwa mradi wa TASAF,barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 1.7 yenye thamani ya shilingi milioni 26.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa Nyumba ya Madaktari inayojengwa katika Sheia ya Kijini,jimbo la Matemwe,Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar yenye thamani ya shilingi milioni 80.Mradi huo huo umejengwa kwa nguvu za Wananchi na Serikali pia.
Na Mwandishi Wetu.

No comments:

Powered by Blogger.