LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATANZANIA WATAKIWA KUJIANDAA VYEMA KUKABILIANA NA USHINDANI AFRIKA MASHARIKI.

Ndaro Kulwijira (Kulia) ambae ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza akifungua Kikao cha Viongozi Kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashari  Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Kilichofanyika Jijini Mwanza. Kushoto ni Amantius Msole Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Watanzania wametakiwa kujiandaa vyema ikiwa ni pamoja na kubadili fikra zao katika kukabiliana na Ushindani wa masuala mbalimbali kutokana na Mtangamano wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hayo yalielezwa juzi Jijini Mwanza katika
Kikao cha Viongozi kutoka Wizara ya Afrika Mashariki, kikao ambacho kiliwajumuisha wadau mbalimbali kutoka Mkoani Mwanza kikiwa na lengo la kujadili kwa pamoja masuala mbalimbali yanayohusiana na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Miongoni Mwa wadau walioshiriki katika Kikao hicho ni pamoja na Wanahabari, Wafanyabiashara, Wajasiriamali pamoja na Wachumi, ambapo katika Kikao hicho pia Mada juu ya Uwepo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliweza kutolewa na baadae washiriki wa Kikao hicho kupata fursa ya Kuchangia mawazo yao.

Akitoa Mada katika Kikao hicho, Amedeus Arbogast Mzee ambae ni Mchumi kutoka Wizara ya Afrika Mashariki alisema kuwa zipo fursa nyingi za uwepo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo Watanzania wajiandae vyema kuzitumia fursa hizo badala ya kuogopa uwepo wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa minajili ya kupoteza furza walizonazo kutokana na Uwepo wa jumuiya hiyo.

Alizitaja baadhi ya Fursa hizo kuwa ni pamoja na Wananchi kufanya Biashara, Kuwekeza, Kuajiriwa pamoja na kupata haki ya Makazi katika nchi yoyote mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hizo zikiwa ni baadhi tu ya fursa miongoni mwa fursa nyingi zilizopo kutokana na Uwpo wa Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki.

Nae Amantius Msole Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki alibainisha kuwa kwa sasa Ushirikiano miongoni Mwa nchi tano zinazounda Jumuiya ya Afrika Masharini ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda ni Mzuri hivyo Watanzania wanapaswa kufahamu kwamba hakuna vikazo vya aina yoyote miongoni mwa nchi hizo hivyo wachangamkie fura mbalimbali zilizopo.

Baadhi ya Washiriki wa Kikao hicho walilalamikia urasimu uliopo katika Mipaka mbalimbali iliyopo katika zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki na hivyo kuomba urasimu huo kuondolewa kwa lengo la kurahisisha shughuli mbalimbali zikiwemo za kibiashara Miongoni mwa nchi zinazounda Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki.

Awali akifungua Kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Naro Kulwijira ambae ni Kaimu Tawala Mkoa wa Mwanza alibainisha kwamba bado Watanzania wengi hawaujui umhimu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na hivyo kuomba elimu zaidi kuendelea kutolewa kwa wananchi juu ya faida na Umhimu wa Jumuiya hiyo kwa lengo la kuzichangamkia fursa zilizopo badala ya kuonekana kujwa na hofu juu ya Uwepo wa Jumuiya hiyo kwa minajiri ya kupoteza fursa zilizopo ambazo ni pamoja na suala la Ajira.

Kikao cha Viongozi kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kilichofanyika jana Jijini Mwanza ni mwendelezo wa Vikao vya Jumuiya hiyo vinavyoendelea katika Miji na Majiji yaliyo Mipakani kwa lengo la kutoa elimu juu ya Umhimu wa Uwepo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo awali vikao hivyo vilifanyika katika miji ya Bukoba na Misenyi Mkoani Kagera na Kukutana na Wadau mbalimbali.
Amantius Msole Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Amedeus Arbogast Mzee ambae ni Mchumi kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, akitoa Mada katika kikao cha Wizara hiyo kilichofanyika Jijini Mwanza na kuwajumuisha wadau mbalimbali ambao ni Pamoja na Wanahabari, Wafanyabiashara, Wajasiriamali pamoja na Wachumi/ Viongozi wa Halmashauri.
Eng. Abdillah Mataka ambae ni Mkurugenzi Msaidizi, Miundominu kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Kushoto) na Kulia ni  Dr.Abdulah Mataka ambae ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Biashara kutoka Wizara hiyo.
Wanahabari wakifuatilia Kwa Makini Mada katika Kikao cha Viongozi kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika Jijini Mwanza.
Baadhi ya Wadau wakifuatilia Kwa Makini Mada katika Kikao cha Viongozi kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika Jijini Mwanza.
Taswira ya Kikao cha Viongozi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wadau mbalimbali kilichofanyika Jijini Mwanza.
Taswira ya Kikao cha Viongozi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wadau mbalimbali kilichofanyika Jijini Mwanza.
Na: George Binagi-GB Pazzo.

No comments:

Powered by Blogger.