LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHEKA AHUKUMIWA JELA KWA KUMPIGA KIBANDA.

CHEKA (KUSHOTO) AKIWA NA SALEH ALLY
Bondia nyota nchini, Francis Cheka ‘SMG’ amehukumiwa miaka mita jela katika Mahakama ya  Mkoani Morogoro.

Taarifa zilizotufikia punde zinaeleza Cheka alipatikana na hatia ya kushambulia baada ya kumpiga aliyekuwa meneja wa baa yake.

Pamoja na kifungo cha miaka mitatu, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakamani
hiyo, Said Msuya amemhukumu Cheka kulipa faini ya Sh milioni moja baada ya kumaliza kifungo hicho.


Cheka alipatikana na hatia ya shambulio dhidi ya aliyekuwa meneja wa baa yake, Bahati Kibanda aliyemshambulia Julai 2, mwaka jana katika Ukumbi wa Vijana Social aliokuwa ameukodi kwa ajili ya kuendesha shughuki za baa zilizokuwa zinasimamiwa na KIbanda.

Kutokana na kukutwa na hatia, Cheka amekuhukumiwa kwenda jela kwa muda huo na imeelezwa tayari ameshapelekwa kwenye gereza mkoani humo.
Na:Salehjembe.

No comments:

Powered by Blogger.