LIVE STREAM ADS

Header Ads

NAHODHA SIMBA AAMUA KUWAFUNGIA MASHABIKI WAO, HASA WALE WATUKUTU


Nahodha wa Simba, Isihaka Hassan amewataka mashabiki kukubali kuungana na timu yao wakati wa shida na raha.
Isihaka aliyasema hayo jana mara tu baada ya kikosi hicho kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu JKT katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Isihaka aliwataka mashabiki wa Simba kuungana.
"Vizuri mashabiki wakajua sisi tunahitaji ushindi ndiyo maana tunakuja kupambana hapa uwanjani.
"Si tukifungwa watu wasiseme wachezaji ni wazembe au viongozi wana matatizo. Badala yake wajue tumeteleza na waungane nasi," alisema.

Alisema wanaendelea kujiandaa vema ili waweze kufanya vizuri hadi mwisho wa ligi.
Mabao yote mawili ya Simba katika mechi hiyo, yalifungwa na Danny Sserunkuma ambaye alipokea pasi mbili za Mganda mwenzake, Emmanuel Okwi.
Na:SalehJembe

No comments:

Powered by Blogger.