LIVE STREAM ADS

Header Ads

MR.MENGI AELEZA ALIVYONUSURIKA KIFO KISA MCHEPUKO.

Msanii Mengi Rukonge a.k.a Mr.Mengi
Wakati leo Februari 14, 2015 tunasherehekea Siku ya Wapendanao Duniani ambayo ni Valentine’s Day, Msanii Mengi Rukonge a.k.a Mr.Mengi ambae anachipukia katika mziki wa Bongo Fleva kwa kasi ya ajabu kutoka Mkoani Mwanza ameelezea namna alivyonusurika kifo huku sababu ikiwa ni kuchepuka nje ya ndoa yake.

Mr.Mengi aliyasema hayo jana wakati akizungumza na BINAGI MEDIA GROUP ikiwa ni wosia wake kwa wapendanao katika kuelekea siku ya Valentine’s Day huku akiwataka kuwa watulivu na wapenzi wako kwa kuwa michepuko niw days si dili maana nusra imuondoe duniani.

Akisimulia kilichompata, Mr.Mengi ambaE ana mke mmoja na Watoto watatu alitonya kuwa ilikuwa mwaka jana ambapo yeye na mke wake walienda kumtembelea mama yao (Mama Mzazi na Mr.Mengi), na  ilipofika usiku marira ya saa mbili yeye alimuacha mkewe kwa mama yake kwa lengo la kurudi nyumbani kwake lakini alipokuwa njiani mipango ilibadilika na hivyo akawasiliana na mchepuko wake kwa lengo la kwenda kujivinjari nao usiku huo.

“Nilikuwa nikitoka kwa mama maeneo ya Nyanguge Magu nikielekea Kasoli Bariadi kwa ajili ya kuonana na Mchepuko wangu huku nikiwa nimekodi pikipiki, lakini kabla sijafika huko tukiwa eneo la nguzo mbili Magu tulipata ajali mbaya sana baada ya pikipiki tuliyokuwa nayo kugonga katika matuta ya barabarani katika eneo hilo. Hakika niliumia sana na hata haya makovu unayoyaona ndugu yangu yalitokana na ajali hiyo” Alitonya Mr. Mengi huku akionyesha makovu aliyonayo mwilini.

Mr.Mengi anasema kuwa baada ya ajali hiyo alijikuta yuko hospitalini na baada ya hapo akatoa taarifa kwa mkewe ambapo alimueleza kuwa yupo hospitalini na amepata ajali mbaya jambo ambalo lilimshtua mkewe ambae alitaka kujua usiku huo alikuwa akienda wapi wakati alimuaga kwamba anaelekea nyumbani nyumbani kulala.

“Baada ya mke wangu kunibana nilikuwa naelekea wapi usiku huo hadi nimepata ajali, ilibidi nimueleze kuwa nilikuwa naenda kutengeneza mashine ya kuchomelea vyuma (Wellding) kwa kuwa ilikuwa imeharibika hivyo nikaona ni vyema nikaitengeneze usiku huo kwa ajili ya kuamkia katika kazi ya uchomeleaji ambayo pia huwa naifanya” Alisema Mr.Mengi na kuongeza kuwa baada ya ajali hiyo aliamua kuachana na michepuka na kutulia na mke wake ambae mpaka sasa wanaishi pamoja kwa uaminifu mkubwa ndani ya ndoa yao.

Akihitimisha inshu hiyo Mr.Mengi aliwashauri wale wote walio katika mahusiano ya ndoa, uchumba au mapenzi kuwa waaminifu na kuepukana na michepuko si tu katika Siku hii ya Valentine’s Day bali katika kipindi chao chote cha mahusiano kwa kuwa mwisho wa kuchepuka ni aibu au mchepukaji kupatwa na visa mbalimbali ambavyo vinaweza kukuondoa uhai wake wa kuishi hapa duniani.

Kumbuka Mr.Mengi kwa sasa anatamba na ngoma mbili ambazo ni NAKUJALI ambapo humo ndani C.SIR MADINI amepewa shavu huku wimbo wa pili ukiwa unaitwa UMEONDOKA na humo ndani wamepewa shavu wasanii MPITA NJIA pamoja na SIHA.

SIKILIZA HAPA CHINI HIZO NGOMA. USHAURI 0764 45 87 77.
NAKUJALI-MR. MENGI ft. C.SIR MADINI.


UMEONDOKA-MR. MENGI ft. SIHA & MPITA NJIA.

Na: George Binagi-GB Pazzo-0757 43 26 94

No comments:

Powered by Blogger.