LIVE STREAM ADS

Header Ads

KONGAMANO KUBWA LA AMANI KUFANYIKA MKOANI MWANZA.

Viongozi wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Kamati hiyo kutoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari juu ya Kongamano kubwa la Amani linalotarajiwa kufanyika tarehe 28.02.2015 katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza, Kongamano ambalo litahitimishwa tarehe hiyo hiyo katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo kutakuwa na Mchezo wa Mpira wa Miguu kati ya Viongozi wa Serikali pamoja na viongozi dini zote mbili za Kikiristo na Kiislamu.
Kamati ya Amani ya Viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikiristo Mkoani Mwanza, imetoa rai kwa Wananchi Mkoani Mwanza sanjari na Mikoa jirani kujitokeza kwa wingi katika kuhudhuria Kongamano kubwa la Amani linalotarajiwa kufanyika Mwishoni Mwa Mwezi huu Mkoani Mwanza.

Rai hiyo ilitolewa hii leo Mkoani Mwanza na Baba Askofu Charles Sekelwa ambae ni Mwenyeki Mwenza wa Kamati hiyo, wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na Kongamano hilo la Amani.

Askofu Sekelwa alibainisha kwamba kongamano hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 28 ya Mwezi huu katika Uwanja wa Furaisha kuanzia majira ya Saa mbili asubuhi hadi saa Saba Mchana, huku akiongeza kuwa Kongamano hilo litahitimishwa katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo kutakuwa na mchezo wa Mpira wa Miguu kati ya Viongozi wa Serikali pamoja na Viongozi wa Dini zote mbili za Kiislamu na Kikiristo kuanzia majira ya saa tisa mchana.

Alisema kuwa lengo la Kongamano hilo la Amani ni kutoa elimu ya Umuhimu wa Amani na Mahusiano kwa Watu na rika zote ili kudumisha amani na utulivu, ambapo alibainisha kwamba elimu hiyo itatolewa na Wanazuoni mbalimbali kutoka dini zote mbili za Kiislamu na Kikristo.

Kaulimbiu katika Kongamano hilo la Amani ni Tunaishi Pamoja, Tunakula Pamoja, Tunacheza Pamoja katika Nchi Moja.

Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini ya Kiislamu na Kikristo Mkoani Mwanza iliundwa tangu mwaka 2013 ikiwa na Wajumbe 20 kwa maana ya Maaskofu 10 kutoka Mabaraza yote ya Kikristo nchini pamoja na Masheikh 10 kutoka Baraza la Bakwata sanjari na Taasisi mbalimbali za Kiislamu.
Kutoka Kulia ni Sheikh Mohamed Salum Balla (Katibu), Sheikh Hassan Kabeke (Mwenyekiti), Baba Askofu Charles Sekelwa (Mwenyekiti) pamoja na Baba Askofu Zenobius Isaya (Katibu) ambao ni Viongozi wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa dini Mkoani Mwanza. Walioko nyuma yao ni Wajumbe wa Kamati hiyo.
Wanahabari waliokuwa katika Mkutano baina yao na Viongozi wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza wakati Kamati hio ikitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari juu ya Kongamano kubwa la Amani linalotarajiwa kufanyika tarehe 28.02.2015 katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza, Kongamano ambalo litahitimishwa tarehe hiyo hiyo katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo kutakuwa na Mchezo wa Mpira wa Miguu kati ya Viongozi wa Serikali pamoja na viongozi dini zote mbili za Kikiristo na Kiislamu.

Viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Manispaa ya Ilemela pamoja na Serikali ya Mkoa wa Mwanza.
Wanahabari waliokuwa katika Mkutano baina yao na Viongozi wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza wakati Kamati hio ikitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari juu ya Kongamano kubwa la Amani linalotarajiwa kufanyika tarehe 28.02.2015 katika Uwanja wa Furahisha Mkoani Mwanza, Kongamano ambalo litahitimishwa tarehe hiyo hiyo katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo kutakuwa na Mchezo wa Mpira wa Miguu kati ya Viongozi wa Serikali pamoja na viongozi dini zote mbili za Kikiristo na Kiislamu.
Na: George Binagi-GB Pazzo

No comments:

Powered by Blogger.