LIVE STREAM ADS

Header Ads

KATIBU WA CCM MKOA WA MWANZA HAKAMATIKI. ATUA WILAYANI KWIMBA KWA KASI YA AJABU.

Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kwimba jana wakiwa katika Kikao na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Hayuko pichani) kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.
 Na:George GB Pazzo
Baadhi wa Watendaji na Watalaamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba wakiwa katika Kikao cha halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilayani humo ikiwa ni katika ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miradi Mtaturu iliyoanza jana Wilayani Kwimba. Ziara hiyo ni ya siku mbili hivyo inatarajiwa kutamatishwa leo katika jimbo la uchaguzi la Sumve.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Aliesimama) akizungumza jana na wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM katika Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza ikiwa ni katika ziara yake ya siku mbili Wilayani Kwimba.
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Pili Moshi Bayo (aliesimama) akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Kwimba ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Kutoka Kushoto ni Issack Kalleiya ambae ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mwanza akifuatiwa na Tabu Lugwesa ambae ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kwimba na wa kwanza Kulia akiwa ni Simon Mayunga Mangelepa ambae ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Mwenye Miwani) akiingia katika Uwanja wa Ngudu Wilayani Kwimba Mkoa wa Mwanza hii leo kwa ajili ya kuhutubia katika Mkutano wa hadhara hii leo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akisalimiana na akina mama wanaounda vikundi mbalimbali vya Ujasiriamali Wilayani kwimba wakati akiingia katika Uwanja wa Ngudu Kwimba kwa ajili ya Mkutano wa hadhara hii leo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akihutubia katika Mkutano wa hadhara hii leo katika Kata ya Ngudu Wilayani Kwimba ikiwa ni katika ziara yake ya siku mbili iliyoanza jana Wilayani Kwimba.
Diwani wa Kata ya Ngudu Feisal Yassin (CCM) akitoa salamu zake katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Stand ya zamani Ngudu Kwimba Mkoani Mwanza ambapo Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (hayuko pichani) alikuwa akihutubia ikiwa ni katika ziara yake ya siku mbili iliyoanza jana na kutarajiwa kuhitimishwa hii leo Wilayani Kwimba.
WanaCCM pamoja na wananchi kwa ujumla wakifuatilia Mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Ngudu Stand ya Zamani Wilayani Kwimba ambapo Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu alikuwa akihutubia katika Mkutano wa hadhara.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akiwakabidhi wachezaji wa Timu ya Kwimba Rangers iliyopo Kata ya Chamela vifaa vya michezo ambavyo ni Mpira mmoja pamoja na Jezi moja vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Sumve Wilayani Kwimba Richard Ndassa lengo likiwa ni kuendeleza michezo Wilayani kwimba.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akiwakabidhi wachezaji wa Timu ya Nyota Fc iliyopo Kata ya Ilumba vifaa vya michezo ambavyo ni Mpira mmoja pamoja na Jezi moja vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Sumve Wilayani Kwimba Richard Ndassa lengo likiwa ni kuendeleza michezo Wilayani kwimba.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akiwakabidhi wachezaji wa Timu ya Mlimani Fc iliyopo Kata ya Ngudu Lugulu vifaa vya michezo ambavyo ni Mpira mmoja pamoja na Jezi moja vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Sumve Wilayani Kwimba Richard Ndassa lengo likiwa ni kuendeleza michezo Wilayani kwimba.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza akiwakabidhi wachezaji wa Timu ya Saloon Fc iliyopo Kata ya Ngudu Mjini vifaa vya michezo ambavyo ni Mpira mmoja pamoja na Jezi moja vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Sumve Wilayani Kwimba Richard Ndassa lengo likiwa ni kuendeleza michezo Wilayani kwimba.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akiwakabidhi Mama Lishe wa Agape Groups wanaopatikana Wilayani Kwimba Mkoa wa Mwanza vyombo vya chakula ambavyo ni Hot Pot kubwa mbili, Food Warmer Moja, Sahani pc 100 pamoja na vikombe vya chai pc 48 vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Sumve Wilayani Kwimba kwa ajili ya kuwawezesha kujiinua kiuchumi.

Akina Mama Lishe wa Agape Groups wanaopatikana Wilayani Kwimba Mkoa wa Mwanza wakiwa na vyombo vya chakula ambavyo ni Hot Pot kubwa mbili, Food Warmer Moja, Sahani pc 100 pamoja na vikombe vya chai pc 48 vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Sumve Wilayani Kwimba kwa ajili ya kuwawezesha kujiinua kiuchumi.
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Pili Moshi Bayo hii leo akiwasalimia wananchi wake katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa stand ya zamani Ngudu Kwimba ambapo Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu alikuwa akiongea na wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho.
Mtatu yuko Wilayani Kwimba kwa ziara ya siku mbili iliyoanza jana na inatarajiwa kuhitimishwa hii leo ambapo pamoja na mambo mengine anatarajia kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo la Uchaguzi Kwimba na Sumve Wilayani Kwimba pamoja na kuzungumza na wananchi pamoja na wanachama wa CCM jimboni Sumve kabla ya kuelekea Wilayani Magu kwa ajili ya kuendelea na ziara zake za kutembelea Wilaya zote za Mkoa wa Mwanza.
SOURCE:RADIO METRO

No comments:

Powered by Blogger.