WATU WATANO WAANGUKIWA NA UKUTA KATIKA ENEO LA UJENZI JIJINI MWANZA.
Mapema hii leo wakati wa zoezi la kuwaokoa watu waliodondokewa na Ukuta wakati wakiwa katika shughuli ya Ujenzi Jijini Mwanza.
Na:Prisca Mshumbuzi
Watu watano wamenusirika kifo
baada ya kudondokewa na ukuta ambao ujenzi wake ulikuwa ukiendelea kujengwa katika eneo la kitalu namba sita, block U barabara ya Nyerere
Jijini Mwanza.
Akizungumza
muda mfupi baada ya tukio hilo, msimamizi
wa ujenzi
huo Williamu Issa alisema kuwa watu hao ambao ni mafundi walikumbwa na tukio
hilo hii leo majira ya saa tano asubuhi, wakati wanafukia sehemu ya ardhi ambayo kulikuwa na mmomonyoko wa udongo na ndipo ghafla ukuta ukawadondokea.
Muuguzi wa zamu kitengo cha
wagonjwa wa dharula hospitali ya rufaa bugando, Dk. Ernest Elisenguo alithibitisha kupokea majeruhi hao
ambapo majeruhi wawili walikuwa katika hali mbaya huku majeruhi akifafanua kuwa
hali za majeruhi watatu hazikuwa mbaya sana hivyo watatibiwa na kuruhusiwa
kurudi nyumbani.
Aliwataja wagonjwa ambao hali yao haikuwa
nzuri kuwa ni Benson Daudi ambaye hali
yake ilikuwa mbaya kiasi cha kupoteza fahamu kutokana na kupata mtikisiko kichwani, Rashidi Mkumba
ambaye amevunjika mguu wa kushoto pamoja na mbavu.
Dr.Elisengue
aliwataja majeruhi watakao ruhusiwa kurudi nyumbani baada ya
matibabu kuwa ni Elias Bahati, Agustino
Msindi na Ramadhani Nyarandu ambao hali yao ilionekana kuimarika wakati wakiendelea kupata
huduma.
Naye Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka
Konisa aliagiza
ujenzi huo usimame hadi pale uchunguzi utakapo kamilika
ili kuweza kubaini chanzo kamili cha kuanguka kwa ukuta huo.
Mapema hii leo wakati wa zoezi la kuwaokoa watu waliodondokewa na Ukuta wakati wakiwa katika shughuli ya Ujenzi Jijini Mwanza.
SOURCE:BINAGI MEDIA GROUP
No comments: