LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAZISHI YA KAPTAINI KOMBA YALIVYONYANYIKA KIJIJINI KWAO LITUHI MKOANI RUVUMA.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndugu Sixtus Mapunda pamoja na wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Tanzania kwenda kumzika marehemu Kapteni John Komba kijijini kwao Lituhi Wialaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma siku ya jana.
Rais Jakaya Kikwete leo amewaongoza viongozi wa serikali, viongozi wa kisiasa na mamia ya watanzania waliojitokeza kuuzika mwili wa aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba Kijijini Lituhi jana.
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Mbinga Mhashamu John Ndimbo akiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma leo.(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa ,Mkoani Ruvuma.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa ,Mkoani Ruvuma.(picha na Freddy Maro).
Jeneza la Kaptaini Komba likiingizwa katika nyumba yake ya Milele.
Mke wa Marehemu Kapteni John Komba ,Salome (kushoto) akiweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu.
Watoto wa marehemu Kapteni John Komba wakiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba yao.
Watoto wa marehemu wakilia kwa uchungu wakati wa kuweka shada la maua kwenye kaburi la Baba yao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete juu ya kaburi la Kapteni John Komba aliyezikwa kwenye makaburi ya kijiji cha Lituhi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima mara baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Komba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Damian Komba aliyezikwa kijijini kwake Lituhi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Lameck Mchemba pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye wakiweka shada la maua juu ya kaburi la Kapteni John Komba aliyefariki jijini Dar es Salaam tarehe 28 februari na kuzikwa kijijini kwake Lituhi tarehe 3 Machi 2015.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Ndugu Said Mwambungu (kulia) akiweka shada la maua pamoja na mkewe kwenye kaburi la Kapteni John Komba.
Khadija Kopa akiwa katika huzuni kubwa mara baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Komba kijijini kwake Lituhi Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.
KWA HISANI YA MTANDAO.
BINAGI MEDIA GROUP; R.I.P KAPTAINI KOMBA.

No comments:

Powered by Blogger.