LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWILI WA KAPTAINI KOMBA WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM KWENDA MKOANI RUVUMA KWA AJILI YA MAZISHI.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kapteni Komba anatarajiwa kuzikwa kijijini Kwake Litui wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.

Na: George Binagi-GB Pazzo
Mwili wa Mbunge wa Mbinga Magharibi Mkoani Ruvuma kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Kapteni John Damiano Komba aliefariki dunia juzi jumamosi akiwa katika Hospitali ya TMJ Jijini Dar es salaam kutokana na chanzo kilichoelezwa kuwa ni tatizo la kisukari umeagwa hii leo katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam kwenda Mkoani Ruvuma kwa ajili ya Mazishi.

Akisoma Wosia wa Marehemu Kapteini Komba, Kaimu Katibu wa Bunge John Joel amesema kuwa Marehemu Kapteini John Damiano Komba alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Shinikizo la damu ambapo takribani wiki mbili kabla ya kifo chake alianza kusumbuliwa na tatizo la Kisukari jambo lililopekelea umauti wake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete ameongoza mamia ya waombolezaji pamoja na Viongozi wa Serikali, dini sanjari na vyama vya Siasa katika kuuaga Mwili wa Kaptaini Komba ambae amesafirishwa kwenda kwenda Ruvuma ambapo pia shughuli ya kuuaga mwili huo itafanyika katika Uwanja wa Majimaji kabla ya kwenda kupumzishwa katika nyumba yake ya milele katika Kiji cha Lituhi Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimfariji mjane wa marehemu Salome Komba katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. Jenista Mhagama akitoa salamu za Serikali wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Rais Kikwete (katikati) akijadiliana jango na Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Wengine pichani toka kushoto ni Rais Mstaafu,Mh. Ali Hassan Mwinyi,Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete pamoja na Rais Mstaafu awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa.
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakiwa kwenye viwanja vya Karimjee leo.
(Picha na Freddy Maro).

No comments:

Powered by Blogger.