SHIRIKISHO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI KANDA YA ZIWA LAZINDULIWA KWA STYLE YA PEKEE.
Na: George Binagi-GB Pazzo
Shirikisho
la Waimbaji wa Muziki wa Injili Kanda ya Ziwa, limezinduliwa Rasmi katika
Uwanja wa CCM Kirumba Ilemela Mkoani Mwanza, ambapo uzinduzi huo uliambatana na
Tamasha kubwa la Marafiki.
Akizungumza jana katika Uzinduzi wa Shirikisho hilo, Idd Juma ambae ni
Mratibu wa Tamasha la Marafiki lililoambatana na Uzinduzi huo alisema kuwa
lengo la kuanzisha Shirikisho la Waimbaji wa Muziki wa Injili Kanda ya Ziwa ni
kuuinua muziki huo sanjari na waimbaji wake hususani katika Mikoa ya Kanda ya
Ziwa na Tanzania kwa ujumla.
Alibainisha kwamba ndani ya Shrikisho hilo kutakuwa na Muungano wa
Vyama mbalimbali ambavyo ni Chama cha Wanakwaya, Chama cha Band za Injili,
Chama cha Waimbaji binafsi, Chama cha Watangazaji wa muziki wa Injili wa radio
na Tv, Chama cha Waalimu wa Kwaya, Chama cha wapiga Muziki wa Injili pamoja na
Chama cha Watengenezaji wa Muziki wa Injili.
Kwa pamoja Juma alisema kuwa vyama hivyo ndivyo vinavyounda Shirikisho
la Waimbaji wa Muziki wa Injili Kanda ya Ziwa, huku akiongeza kuwa ili Muziki
wa Injili uweze kupiga hatua zaidi, Shirikisho hilo limeadhimia kuanzisha
Studio kwa ajili ya kuwasaidia waimbaji wa Muziki wa Injili kurekodi kazi zao
kwa gharama nafuu.
Aidha Juma alitoa rai kwa Watanzania kuipigania na kuendelea kuienzi
amani ya Tanzania huku akikemea vitendo vya Utekaji na Mauaji ya Watu wenye
Ulemavu wa ngozi ambavyo vimeonekana kushamiri hapa nchini hususani katika
Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Mgeni Rasmi katika Tamasha hilo la Marafiki Dede Petro ambae ni
Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Daladala Kanda ya Ziwa, alitoa rai kwa
waimbaji wa Muziki wa Injili ya Ziwa kuendelea kushikamana kwa pamoja ambapo
pamoja na mambo mengine alichangia Shilingi Laki Tano kwa ajili ya kusaidia
Shirikisho hilo la Waimbaji wa Muziki wa Injili Kanda ya Ziwa.
Wakishiriki katika kuchangia harambee ya kuimarisha Shirikisho hilo la
Waimbaji wa Muziki wa Injili, Dede Swila Dede ambae ni Diwani wa Kata ya Mgogwa
na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela pamoja na Sarah Paul Ng’wani ambae ni
diwani Viti Maalumu katika Manispaa hiyo, waliwasihi Watanzania kuhakikisha
kwamba wanailinda Amani ya Tanzania hususani katika kipindi hiki cha kuelekea
katika Uchaguzi Mkuu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba utekaji na mauaji ya
watu wenye ulemavu wa ngozi yanatokomezwa mara moja.
Idd Juma ambae ni Mratibu wa Tamasha la Marafiki lililofanyika jana katika Uwanja wa CCM Kirumba Ilemela Mkoani Mwanza. |
Dede Swila Dede ambae ni Diwani wa Kata ya Mgogwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. |
Sarah Paul Ng’wani ambae ni diwani Viti Maalumu katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. |
Joseph Boniface (wa kwanza kulia) ambae ni Marketing Manager Kampuni ya Proin Promotion Mwanza. |
No comments: