LIVE STREAM ADS

Header Ads

UKAWA TAWI LA CAPRIPOINT JIJINI MWANZA KUTOSHIRIKI KURA YA MAONI YA KATIBA MPYA.

Na: George Binagi-GB Pazzo
Wakati Serikali inaendelea na zoezi lake la usambazaji wa nakala za rasimu ya Katiba Mpya inayopendekezwa, Suala la Ushiriki wa Kura ya Maoni ya Katiba hiyo bado limeendelea kuwa katika hali ya Mvutano kwa baadhi ya Vyama vya  Siasa hapa nchini, hususani kwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa.
Juzi Daud Msangya ambae ni Mwenyekiti wa Ukawa Tawi la Capripoint na Serikali ya Mtaa wa Capripoint Jijini Mwanza kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, alibainisha kuwa Ukawa tawi la Capripoint itaendelea na Msimamo wake wa kutoshiriki katika Kura hiyo ambayo inatarajiwa kupigwa April 30 Mwaka huu ikiwa ni msimamo unaotokana utekelezaji wa kauli ya Viongozi wa Ukawa ngazi ya Taifa ambao wanasisitiza Kura ya hapana dhini ya Katiba hiyo pendekezwa.
Alisema kuwa maamuzi hayo yametokana na namna ambavyo maoni ya wananchi yaliyokuwa katika Rasimu ya iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya yalivyochakachuliwa na lililokuwa bunge Maalumu la Katiba Mpya.

Aidha aliongeza kuwa suala la uwepo wa Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa kuungana katika Uchaguzi Mkuu halitakuwa na ugumu wowote katika kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi, japo ametahadharisha kwamba lolote laweza kutokea na kusababisha malumbano ndani ya Umoja huo wa Ukawa katika kipindi cha kuwatafuta wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi Mkuu ujao.

No comments:

Powered by Blogger.