LIVE STREAM ADS

Header Ads

WIZARA YA MADINI YAJIPANGA KUKUZA ZAIDI PATO LA TAIFA, WANANCHI

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com 
Wizara ya Madini imejipanga ili kuhakikisha mchango wa sekta ya madini unaendelea kukua na kuwanufaisha wananchi pamoja na kukuza zaidi pato la Taifa.

Hayo yamebainishwa Alhamisi Novemba 20, 2025 na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo wakati akifungua mkutano wa  kwanza wa mwaka wa fedha 2025/26 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika jijini Mwanza.

Mbibo amesema ili kutimiza lengo hilo, Wizara imeweka vipaumbele mbalimbali ikiwemo kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli, kukuza mnyoro wa thamani katika sekta ya madini muhimu na ya kimkakati, kuwarasimisha na kuwaendeleza wachimbaji wadogo nchini.

"Tutahamasisha uwekezaji na uongezaji thamani madini, kuendelea kufanya tafiti za kina za madini na kuimarisha uendeshaji wa minada na maonesho ya madini ya vito pamoja na kuzijengea uwezo taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi" alisema Mbibo.

Mbibo alibainisha kuwa katika kipindi cha mwezi Julai hadi Oktoba mwaka huu 2025, Wizara imefanikiwa mafanikiwa kukusanya maduhuli ya shilingi bilioni 430.1 sawa na asilimia 35 ambapo lengo ni kukusanya shilingi trilioni 1.19 kwa mwaka wa fedha 2025/25.

Pia Mbibo amebainisha kuwa uwepo wa Baraza la Wafanyakazi katika sehemu za kazi ni matakwa ya kisheria, hivyo amehimiza wajumbe baraza hilo kutoa maoni na mapendekezo yatakayosaidia Wizara kufanya vizuri katika utekelezaji wake wa majukumu.

Naye Katibu wa Chama cha Wafanyakazi Tanzania (TUGHE) Mkoa wa Mara, Hamisi Mwisa akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, ametoa rai kwa wafanyakazi Wizara ya Madini waluoshiriki mkutano huo kutoa maoni yatakayosaidia kuboresha ufanisi kazini hatua itakayosaidia pia kubiresha maslahi yao kazini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Madini.

No comments:

Powered by Blogger.