PUMZIKA KWA AMANI KAPTENI KOMBA. WATANZANIA WATAKUKUMBUKA NA HII KAULI YAKO.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Mbunge wa Mbinga
Magharibi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Kapteni John Damian Komba
amefariki dunia hii leo akiwa katika Hospitali ya TMJ Jijini Dar
es salaam ambapo chanzo cha kifo
chake kimeelezwa kuwa ni kutokana na tatizo la kisukari alilokuwa nalo.
Mbali ya kuwa mwanasiasa pia Komba ndiye aliyekuwa kiongozi wa
kundi la TOT sanjari na kuwa msanii aliekuwa akiimba kwaya katika kundi hilo
ambalo lilijumuisha sanaa mbalimbali zikiwemo kwaya, dansi, sarakazi pamoja na
taarabu.
Kapteini Komba ambae pia alikuwa ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya
Taifa ya CCM miongoni mwa kauli zake zitakazokumbukwa ni pamoja na kauli yake
aliyoitoa enzi za uhai wake wakati akihojiwa katika kipindi cha Mkasi Tv kinachoruka EATv ambapo
alipoulizwa ni mwanasiasa gani anastahili kuwa rais wa Tanzania kupitia chama
chake cha CCM alisema kuwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edwan Lowasa anafaa kuwa
rais.
‘’...Mimi hapa nilipo leo ukiniuliza nani anafaa kuwa rais, mimi
nasema Lowasa anafaa kuwa rais kamili eeeeeh nitasema Edwad Lowasa anafaa kuwa
rais kabisa. Kama chama changu kitampendekeza mimi mia kwa mia kabisa...’’.
Pumzika kwa Amani Kapteini Komba lakini umeondoka katika kipindi
ambacho pengine ulitakiwa kusalia hapa duniani ili kuweza kushuhudia na kujionea
kauli uliyoitoa juu ya nani anastahi kuwa rais wa Tanzania kupitia chama chako cha CCM kama ingeweza kutimia
kuwa kweli ama la!
No comments: