LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA MKOA WA MWANZA AZUIA MACHINGA KUONDOLEWA ENEO LA IGOMA STAND JIJINI MWANZA.

Baadhi ya Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) wanaofanya biashara zao katika eneo la Igoma Stand Jijini Mwanza wakifurahia Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (Aliejukwaani) ya kuzuia Machinga hao kuondolewa katika eneo hilo kama ambavyo Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ulivyokuwa umekusudia.
 Na:George Binagi-GB Pazzo
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo amezuia Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) wanaofanyia biashara zao katika eneo la Igoma Stand Jijini Mwanza kuondolewa katika eneo hilo kama ilivyokuwa imeagizwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Mulongo alitoa Kauli hiyo Jumamosi iliyopita katika Mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza, ukiwa na lengo la kupata kauli yake kuhusiana na machinga kuzuiliwa na Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kufanyia biashara zao katika eneo la Igoma Stand huku kukiwa hakuna eneo jingine stahiki lililoandaliwa kwa ajili ya wao kufanyia shughuli zao za kibiashara.

Baada ya Mulongo kuelezwa na Machinga waliokuwa katika eneo hilo la Igoma Stand kuwa wametakiwa kuondoka katika eneo hilo bila kuandaliwa eneo jingine la Kufanyia biashara zao, Mulongo alipanda jukwaani na bila kung'ata maneno akatamka wazi kuzuia machinga hao kuondolewa katika eneo hilo bila kuandaliwa eneo jingine la kwenda kufanyia biashara zao.

Katika hatua nyingine Mulongo aliiagiza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuweka taa katika eneo hilo la Igoma Stand kwa lengo la kuwaondolea wafanyabiashara (Machinga) katika eneo hilo adha ya kufanyia shughuli zao gizani nyakati za jioni.

Awali Mwenyekiti wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza Said Tembo alieleza kuwa machinga wamepitia matatizo mengi ambayo yalihatarisha maisha yao hivyo kwa hivi sasa hawako tayari kurudia katika matatizo hayo, hivyo wako tayari kukaa na viongozi wa mbalimbali kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili.                          
Baadhi ya Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) wanaofanya biashara zao katika eneo la Igoma Stand Jijini Mwanza wakifurahia Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (Hayuko pichani) ya kuzuia Machinga hao kuondolewa katika eneo hilo kama ambavyo Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ulivyokuwa umekusudia.
Kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula ambae pia ni diwani wa Kata ya Mkolani (CCM) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Machinga Mkoa wa Mwanza tawi la Igoma Stand Jijini Mwanza. Mabula alikuwa miongoni mwa viongozi waliohudhuria Mkutano wa Hadhara ulioandaliwa na Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza uliokuwa umelenga kupata kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo kama waondoke katika eneo hilo ama waendelee kufanya biashara zao katika eneo hilo la Igoma Stand.
Mwenyekiti wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza Said Tembo (Kushoto) akizungumza katika Mkutano wa hadhara baina ya Machinga wanaofanya biashara zao katika eneo la Igoma Jijini Mwanza. Kushoto ni Mc wa Mkutano huo.
Mwenyekiti wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza Said Tembo (Mwenye Kinasa Sauti) akiwatambulisha viongozi wa Muungano huo Tawi la Igoma Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akisoma Risala ya Machinga tawi la Igoma baada ya kuwasili katika eneo la Igoma Stand kwa ajili ya Mkutano wa Hadhara ulioandaliwa na Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza kwa lengo la kupata kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza baada ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuwataka Wafanyabiashara ndogondogo kuondoka katika eneo hilo. Akizungumza katika Mkutano huo Mulongo aliwapa ridhaa machinga hao kuendelea na shughuli zao kama kaida hadi pale watakapoandaliwa eneo jingine la kufanyia shughuli zao.
Viongozi mbalimbali wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza.
Akina Mama wanaofanya shughuli zao za Ujasiriamali katika eneo la Igoma Stand Jijini Mwanza wakimpa zawadi ya Matunda Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (Kushoto) baada ya kuwaruhusu kuendelea na shughuli zao katika eneo hilo. Awali wafanyabiashara ndogondogo walitakiwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutofanyia shughuli zao katika eneo hilo la Igoma Stand Jijini Mwanza.
Akina Mama wanaofanya shughuli zao za Ujasiriamali katika eneo la Igoma Stand Jijini Mwanza wakimpa zawadi ya Matunda Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo baada ya kuwaruhusu kuendelea na shughuli zao katika eneo hilo. Awali wafanyabiashara ndogondogo walitakiwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutofanyia shughuli zao katika eneo hilo la Igoma Stand Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akiagana na Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) wanaofanya shughuli zao katika eneo la Igoma Stand Jijini Mwanza baada ya kukutana nao katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Juzi Jumamosi ukiwa umelenga kujua hatima ya Machinga hao baada ya awali kutakiwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuondoka katika eneo hilo, ambapo katika Mkutano huo Mulongo alizuia Machinga hao kuondolewa katika eneo hilo kutokana na eneo jipya la wao kwenda kufanyia shughuli zao kutoandaliwa.
CHANZO:RADIO METRO

No comments:

Powered by Blogger.