KATIBU WA CCM MKOA WA MWANZA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA AJILI YA ZIARA YA KIKAZI.
Katibu Wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu (Mwenye Skafu) akisalimiana na viongozi wa Chama hicho baada ya Kuwasili jana jioni Mjini Nansio Wilaya Ukerewe kwa ajili ya ziara yake ya siku mbili inayoanza hii leo. Kulia ni Mwenyeji wake Ally Hamis Mambile ambae ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ukerewe.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Katibu
wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu jana jioni amewasili Mjini
Nansio Wilayani Ukerewe, kwa ajili ya ziara ya kikazi inayotarajiwa kudumu kwa
takribani siku mbili.
Baada ya kuwasili Mjini humo majira ya jioni, Mtaturu alikutana na
Viongozi mbalimbali wa CCM Wilayani Ukerewe, wakiwemo Viongozi wa Mashina,
Matawi, Kata pamoja na Wilaya.
Akizungumza na Viongozi hao, Mtaturu alibainisha kuwa Chama cha
Mapinduzi kinakemea vikali tabia ya baadhi ya Viongozi wa dini hapa nchini,
ambao wamekuwa wakitoa matamko mbalimbali yanayoashiria kuwashinikiza waumini
wa madhehebu yao kupingana na katiba inayopendekezwa.
“Yamekuwa yakitoka matamko, kiukweli sisi kama Chama cha Mapinduzi
tunaona kwamba Viongozi wetu wa Kiroho wameacha kazi yao, wanafanya kazi ya
kisiasa kitu ambacho siyo sawasawa”. Alisema Mtaturu huku akiongeza kuwa badala
ya viongozi hao kuzungumzia Katiba wamekuwa wakiruka zaidi na kupiga kampeni za
uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Octoba mwaka huu 2015.
Mtaturu aliwatahadharisha Viongozi wa dini kwamba wasidhani wanapokuwa
madhabahuni waumini wote wanawaunga mkono kwa mambo wanayofanya, kwani waumini
wengi wamekuwa wakiguna kutokana na matamko mbalimbali ambayo yamekuwa
yakitolewa na viongozi wa dini.
Kauli ya Mtaturu imejili siku chache baada ya Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania katika waraka wao kuishauri Serikali kuwa zoezi la kuipigia kura Katiba nayopendekezwa liahirishwe na kufanyika baada ya Uchaguzi Mkuu, Oktoba mwaka huu kutokana na wananchi wengi kutofikiwa na nakala za Katiba hiyo inayopendekezwa
ambapo baraza hilo lilisema kuwa si jambo la busara kuendelea kuwataka watu kukipigia
kura kitu wasichokijua huku waraka huo ambao ulikusudiwa kusomwa mbele ya waumini pia ukieleza kwamba ikiwa watawala wataendelea kulazimisha kura ya katiba inayopendekezwa kuwepo, basi wananchi wajitokeze na
kupiga kura ya hapana.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu inatarajia kuanza rasmi Wilayani Ukerewe hii leo, ambapo anatarajia kufanya Kikao cha pamoja na Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi, Kukutana na halmashauri kuu ya Wilaya na kupokea taarifa yake na hatimae baadae kufuatiwa na Mazungumzo na Wazee Wilayani Ukerewe.
Ziara ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu inatarajia kuanza rasmi Wilayani Ukerewe hii leo, ambapo anatarajia kufanya Kikao cha pamoja na Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi, Kukutana na halmashauri kuu ya Wilaya na kupokea taarifa yake na hatimae baadae kufuatiwa na Mazungumzo na Wazee Wilayani Ukerewe.
Katibu Wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu (Mwenye Skafu) akisalimiana na viongozi wa Chama hicho baada ya Kuwasili jana jioni Mjini Nansio Wilaya Ukerewe kwa ajili ya ziara yake ya siku mbili inayoanza hii leo. Kulia ni Mwenyeji wake Ally Hamis Mambile ambae ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ukerewe.
Katibu Wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mwanza Miraji Mtaturu (Mwenye Skafu) akisalimiana na viongozi wa Chama hicho baada ya Kuwasili jana jioni Mjini Nansio Wilaya Ukerewe kwa ajili ya ziara yake ya siku mbili inayoanza hii leo. Kulia ni Mwenyeji wake Ally Hamis Mambile ambae ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ukerewe.
Mapokezi kwa ajili ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kushoto) yakiendelea Mjini Nansio Ukerewe.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (Kulia) akisaini daftari la wageni baada ya kuwasili katika ofisi za chama hicho Wilayani Ukerewe. kushoto ni Ally Hamis Mambile amba ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ukerewe.
Abubakar Ghati akisoma taarifa ya Chama cha Mapinduzi Wilayani Ukerewe.
Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Ukerewe.
Mapokezi ya Katibu wa CCM Mkoani Mwanza Mijaji Mtaturu yalipokelewa na kupambwa pia kwa ngoma baada ya kuwasili Bandarini Mjini Nansio. Mbali ya ziara hiyo kuwa ya Kikazi, pia ni maalumu kwa Mtaturu kujitambulisha kwa wanachama baada ya kuwasili hivi karibuni Mkoani Mwanza kama kituo chake kipya cha kazi.
CHANZO: RADIO METRO
No comments: