Miongoni mwa Nyumba zilizobomolewa Wilayani Kahama Mkoa wa Sinyanga kutokana na Mvua ya Mawe iliyonyesha Usiku wa Kuamkia leo March 04, 2015 na Kusababisha vifo vya Watu zaidi ya 38 huku wengine zaidi ya 60 wakijeruhiwa. Pia mvua hiyo imesababisha uharibifu wa mazao pamoja na mifugo kufariki. Wananchi wengi pia wamekosa makazi kufuatia mvua hiyo.
Mvua hiyo ambayo ilinyesha kwa muda mfupi imewaacha watu 3,500 bila makazi katika kaya 350 huku nyumba zikifurika maji na baadhi ya mifugo ikisombwa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bw. Ali Nasoro Rufunga amesema mvua hiyo ya mawe iliyoambatana na upepo mkali ilisababisha mafuruko katika kata ya Mwakata kuezua nyumba na nyingine kuanguka.
Amesema mali mbalimbali zimeharibiwa vibaya ikiwemo mifugo kuzolewa na maji na vyakula kwenye eneo lote lililokumbwa na mafuriko hayo.
Hali ya majeruhi ambao wamepelekwa katika hospitali mbalimbali bado sio nzuri kwa baadhi ingawa wengine wanaendelea vizuri.
|
No comments: